habari Mpya


UNESCO -Waandishi wa Habari 73 wamefariki Wakitekeleza Majukumu Yao.

Na Maria Philbert – RK Mwanza. 


Shirika la kimataifa linalojishughulisha na Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO  kupitia tume ya taifa ya shirika hilo  limesema kuwa   Waandishi wa Habari 73 wamefariki   kwa miaka miwili  iliyopita kwenye nchi za kusini mwa jangwa la sahara wakitekeleza majukumu  yao.

Hayo yameeleza na Katibu Mtendaji wa tume hiyo DK MOSHI KIMIZI akitoa taarifa katika mafunzo ya waandishi wa habari juu ya ulinzi na usalama wa waandishi wa habari wanapotekeleza majukumu yao kutoka mikoa 7 ya kanda ya ziwa yanayoratibiwa na UNESCO.


DK KIMIZI amesema   kwa miaka kumi iliyopita waandishi wa habari 820 wamepoteza maisha duniani kote wakati wa kutekeleza majukumu ya uandishi huku wakiwajibika kufanya kazi kwa ufanisi.

Kwa upande wake Katibu tawala wa Mkoa wa Mwanza Injinia WARIOBA SANYA amewataka baadhi ya wamiliki wa vyombo vya habari  kuboresha mazingira ya kiusalama kwa   waandishi wa habari wanapokuwa kwenye majukumu yao.

Post a Comment

0 Comments