habari Mpya


Serikali yaanza Mchakato wa Kutatua Tatizo la Maji Mkoani Kagera.

Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Bw Juma Awesu amesema Serikali kupitia Wizara hiyo imeanza mchakato wa kutatua tatizo la maji kwenye maeneo ya wilaya mbalimbali za Mkoa wa Kagera.

Bw Awesu ametoa kauli hiyo Jana September 5,2018 Bungeni Jijini Dodoma kwa niaba ya Waziri wa Maji na Umwagiliaji  Dk Isack Kamwelwe akijibu swali la Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Kagera Bi Halima Bulembo kuhusiana na mikakati ya wizara na serikali ya kutafutia ufumbuzi tatizo la maji mkoani humo  kwa kutumia maji ya ziwa Victoria.

Bw Awesu amesema tayari serikali imeanza kulishughulikia tatizo la maji kwenye mkoa huo ambapo tayari imekamilisha mradi wa maji katika manispaa ya Bukoba na maeneo Jirani. 


Licha ya kuuliza swali hilo Bi Bullembo ameishauri serikali kutumia uwepo wa ziwa Victoria mkoani Kagera kuanzisha mradi mkubwa wa maji na chanzo cha kudumu cha maji ambao upo jirani na ziwa victoria ukilinganisha na mkoa wa Tabora.

Post a Comment

0 Comments