habari Mpya


Serikali Kigoma yaanza Kuziba Makorongo ya Mtaa wa Mlole yanayodaiwa Kutumika Kihalifu.

Na Adrian Eustus -RK Kigoma.

Kufuatia ongezeko la matukio ya uhalifu katika mtaa wa Mlole kata ya Mwanga Kaskazini manispaa ya Kigoma ujiji mkoani Kigoma serikali imeanza kuziba Makorongo ya mtaa huo yanayodaiwa kutumiwa na wahalifu katika shughuli zao mbalimbali.

 Diwani wa kata ya Mwanga Kaskazini Bw.Revocatus Chipando amesema mtaa wa Mlole umekuwa na Makorongo kwa zaidi ya miaka Ishirini iliyopita hali inayotishia usalama wa nyumba za wananchi wanaozunguka korongo hilo na mtaa kwa ujumla.

Moja ya Lori la Mchanga linalosomba Vifusi kufukia Makorongo ya mtaa huo yanayodaiwa kutumiwa na wahalifu katika shughuli zao mbalimbali.
Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa wa Mlole Bw.Die Paulo amesema kuzibwa kwa Korongo hilo kutapunguza wimbi la watoto wanaocheza kamali katika Korongo hilo na kwamba wazazi na walezi hawana budi kuwaonya watoto wao wanaotumia muda mwingi kucheza kamali badala ya kusoma.

Baadhi ya wananchi wa mtaa wa Mlole wameipongeza serikali kwa hatua hiyo ambayo wamedai itasaidia kupunguza ongezeko la matukio ya kiuhalifu na kwamba wamekuwa wakishindwa kutumia baadhi ya njia zinazozunguka Korongo hilo kwa kuhofia maisha yao.


Post a Comment

0 Comments