habari Mpya


Rais Magufuli -''Ujenzi wa Meli Mpya Kanda ya Ziwa Utapunguza Gharama za Usafirishaji''.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono wakati akiwasili katika eneo la Bandari la Mwanza South.


Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli amesema kukamilika kwa ujenzi wa meli mpya, chelezo na ukarabati wa meli mbili katika ziwa Victoria kutapunguza gharama za usafirishaji.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo Jana September 3, 2018 baada ya uzinduzi wa zoezi la utiliaji saini mikataba 4 ujenzi wa meli mpya , chelezo na ukarabati wa meli mbili ya Mv Butiama na Mv Victoria wenye thamani ya takibani shilingi bilioni 152 .

Amesema ujenzi wa meli, chelezo na  ukarabaiti wa meli hizo mbili  ni pesa za wananchi na serikali imefikia uamuzi wa kuyafanya hayo ili kurahisisha na kupunguza gharama za usafirishaji wa bishaa mbalimbali na kukamilika kwake kutasaidia kupunguza changamoto za usafirishaji kwa kutumia meli kwenye ziwa victoria.

BOFYA PLAY HAPA CHINI KUMSIKILIZA RAIS DR.MAGUFULI.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia zoezi la utiaji saini Mikataba mbalimbali ikiwemo Ujenzi wa Meli mpya ya abiria na mizigo, Chelezo, ukarabati wa Meli za Mv Victoria na Mv Butiama, Mikataba ambayo ilisainiwa kati ya Kampuni ya Huduma za Meli Tanzania Marine Services Company (MSCL) na Kampuni tatu za Korea Kusini ambazo ni M/S STX engine Co ltd, Saekyung Construction ltd na KTMI Co ltd.

Awali aktoa maelezo ya mikataba hiyo kabla ya kusainiwa Meneja wa Kamuni ya Huduma za Meli hapa Nchini Bw Erick Hamis amemueleza Rais Magufuli kuwa meli hiyo kubwa itakuwa na uwezo wa kubeba watu takribani 1,200 na tani 400 za mizigo pamoja na magari madogo 20.

BOFYA PLAY HAPA CHINI KUMSIKILIZA BW.HAMIS.

Post a Comment

0 Comments