habari Mpya


Idadi ya vifo katika ajali ya kuzama kwa kivuko jijini Mwanza yafika 86

Habari picha hii hapo juu kivuko cha Mv.Nyerere kilichozama katika ziwa Victoria wakati kikieklekea kisiwa Ukara wilayani Ukerewe.
Mwanza.
Saa zaidi ya 20 tangu kuzama kivuko cha MV Nyerere, idadi ya watu waliokufa imefikia86, Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,John Mongella hadi leo saa 4asubuhi Septemba 21, 2018 jumla ya maiti 86 zimeopolewa.


Akihojiwa na  Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), Mongella amesema
miili 42 imepatikana leo asubuhi, wakati mingine 44 ilipatikana jana.

“Watu 40 wameokolewa wakiwa hai, bado tunaendelea na zoezi la uokoaji,”
amesema Mongella.


Zoezi la uokoaji likiendelea kuongozwa na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliani, Isack Kamwelwe, Mkurugenzi wa
Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Boaz na Mkuu wa Jeshi la
Polisi nchini, Inspekta Jenerali  Simon Sirro


Katika zoezi hilo la uokoaji, Mongella amekuwa akitoa maelekzo ya mahali
pa kuhifadhia miili, ambayo inapelekwa katika kituo cha afya cha Bwisya
kilichopo umbali wa mita takribani 300 kutoka kilipozama kivuko hicho.

Kivuko hicho kilizama katika Ziwa Victoria mita 50 kabla ya kutia nanga
kisiwa cha Ukara Kilikuwa kikitokea katika Kisiwa cha Bugolora kuelekea Kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe, kinadaiwa kilikuwa kimepakia zaidi ya abiria 100,
wengi wakiwa wanaelekea kwenye gulio.

Post a Comment

0 Comments