habari Mpya


Gaguti apiga Marufuku Sukari ya Magendo Mkoa wa Kagera.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali MARCO ELISHA GAGUTI ameahidi kuongeza jitihada za kukomesha vitendo vya wafanyabiashara kuingiza Sukari toka nje ya nchi kwa njia ya magendo kupitia mpaka wa mkoa huo na nchi za Rwanda, Burundi, Uganda na Kenya ili kukinusuru kiwanda hicho.
Ametoa kauli hiyo wakati wa ziara yake akitembelea kiwanda hicho September 18,2018 na kupata fursa ya kujionea mashamba ya miwa na kiasi kikubwa cha sukari kwenye maghala huku Meneja Mkuu wa Kiwanda hicho ASHWIN RANA akisema lengo la uzalishaji katika msimu huu ni tani zaidi ya elfu 85.

Aidha Brigedia Jenerali GAGUTI ametoa ushauri kwa uongozi wa kiwanda hicho kuongeza idadi ya mawakala watakaopewa jukumu la kusambaza sukari katika maeneo mbalimbali yaliyoko mkoani Kagera na mikoa ya jirani ili sukari inayozalishwa na kiwanda hicho isambazwe katika maeneo mengi.

Mwanahabri wetu SAMUEL LUCAS amezungumza na Mkuu huyo wa Mkoa wa Kagera ili kujua mkakati uliopo katika Kudhibiti Bidhaa za Magendo Kuingia Nchini kupitia Mkoa wa Kagera.
Kiwanda cha Sukari Kagera tangu kuanza uzalishaji wa sukari katika msimu wa mwaka huu 2018/2019 mwezi Julai tayari kimezalisha jumla ya tani 26,000 za sukari na matarajio ya uzalishaji kwa msimu mzima ni tani 84,000 za sukari. 

Aidha, tani 12,800 za sukari bado hazijaingia sokoni  na bado zipo katika kiwanda hicho kutokana na tatizo la sukari ya magendo katika masoko.

Post a Comment

0 Comments