habari Mpya


‘’Fedha za Maabara moto Ngara,Upasuaji wa Ajabu Misenyi’’-Sikiliza hapa Yaliyojiri September 04.

Ni Jumanne ya Tarehe 4.09.2018, Kutoka Ngara Kagera Tanzania, Hii Ni Radio Kwizera FM, Karibu Katika kipindi cha Yaliyojiri Ambapo unapata nafasi ya kufahamu mambo mbalimbali yaliyo jiri katika Maeneo yetu.


Watu wanne wa familia moja Kata ya Kalela Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma wamepandishwa kizimbani kwa tuhuma za kumshambulia na kumjeruhi kikatili mtumishi wao wakimtuhumu kuiba shilingi laki nne za familia hiyo.


Kutoka Wiliayani Kasulu Mkoani Kigoma Mwanahabari wetu Albert Kavano anaundani wa taarifa hii.


Wakazi wa Mtaa wa Bwinuka Ngoma uliopo kata Kahororo manispaa ya Bukoba mkoani Kagera wameitaka serikali kuwafukuza wanyama waharibifu aina ya Ngedere wanaoharibu mazao yao na kupelekea kuvuna chini ya matarajio yao.Mwanahabari Wetu Anord Kailembo anataarifa zaidi Kutoka manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera.
Watu wanne wanashikiliwa na Jeshi la polisi Mkoani Geita  baada ya kukutwa wakipanga mahari ya binti mdogo mwenye wa umri  miaka kumi na nne.Kutoka Mkoani Geita Mwanahabari Gibson Mika anataarifa zaidi.Wananchi wa kijiji cha Nyamwilonge kata ya Nyamtukuza wilayani kakonko mkoani kigoma  wamewalalamikia wawekezaji wa mgodi wa Nyamwilonge kwa kuwang’olea mazao yao yaliyopo jirani na mgodi huo kwa madai kuwa wanaingilia vitalu vyao.Taarifa yake Mwanahabari wetu Faraja Marko inafafanua kwa kina kutoka Wilayani Kakonko Mkoani Kigoma.Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya maendeleo ya Kibiashara hapa Nchini  Edwin Rutageruka amewataka wakurugenzi wa halimashauri katika maeneo mbalimbali kote Nchini kuhakikisha wanawawezesha wazarishaji wa mazao  ya biashara katika kutatua changamoto ya masoko.Kutoka Wilayani Chato Mkoani Geita Mwanahabari wetu Elias Zephania anaundani wa taarifa hii.Diwani wa kata ya Kanazi wilayani Ngara Bw.Mathias Mugatta ameiagiza bodi ya shule kwakushirikiana na uongozi wa shule ya Sekondari Kanazi kujitathimini juu ya usimamizi wa ujenzi wa maabara 3  katika shule hiyo.Taarifa yake Mwanahabari wetu Juventus Juvenary Inafafanua kwa kina kutoka wilayani Ngara Mkoani Kagera.Katika hali isiyokuwa kijana mmoja  mkazi wa   Wilaya ya Kerwa mkoani Kagera amefikishwa katika hospitali ya Mugana iliyoko wilayani Missenyi  na kufanyiwa upasuaji na kukutwa na vifaa  mbalimbali ikiwemo  mswaki,kijiko ,kalamu ,viberti  vya gesi pamoja na mkonga wa mashine ya kunyolea ndevu.

Kwa undani wa taarifa hii mwanahabari wetu Wiliam Mpanju anafafanua kwa kina kutoka wilayani Missenyi Mkoani Kagera.

Post a Comment

0 Comments