habari Mpya


DC Ngara-''Waacheni Watoto Washindwe Mtihani Msifanye Udanganyifu''.

Epukeni mazingira ya kujaribiwa kwa lengo la kuwasadia watahiniwa; kama hamkuwafundisha vizuri waacheni washindwe, kwa sababu itakuwa ndiyo haki yao.” Mkuu wa Wilaya ya Ngara mkoani Kagera,Lt. Col. Michael Mntenjele akitoa wito huo kwa washiriki wa kazi maalumu Septemba 04, 2018.

Mkuu huyo wa Wilaya ya Ngara Lt. Col. Mntenjele, amesema watoto waliojifunza kwa bidii waachwe wafaulu kwa juhudi zao, huku akiwataka washiriki wa kazi hiyo maalumu kuwa wautulivu, wenye akili pamoja na busara.

Hakikisheni sifa nzuri ya Wilaya ya Ngara inaendelea kudumishwa, na kuhakikisha hakuna udanganyifu katika mithani kwa kusimamia vema mtihani huu.” Alisema Lt. Col. Michael Mntenjele.

Hata hivyo, alisisitiza kwamba anatumaini washiriki hao, wataifanya kazi hiyo nyeti ya kitaifa kwa uadilifu mkubwa, na kwa kuzingatia maelekezo ya kusimamizi mitihani yaliyotolewa na Baraza la Mitihani la Tanzania.

Aidha, amesema uteuzi wa washiriki hao, umezingatia mwongozo na taratibu ambao unasisitiza mshiriki lazima awe na sifa zinazokubalika, ambazo ni kuwa mwaminifu na mwadilifu, uzoefu kazini, afya njema, sifa za kitaaluma pamoja na kufanya shughuli hii kwa kuzingatia maadili ya ualimu.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara na Mwenyekiti wa Kamati ya Mitihani (W) Bw. Aidani John Bahama, ametoa wito kwa wasimamizi wa mitihani wa darasa la saba mwaka huu 2018, kuwa watulivu vituoni na kuacha tabia ya ulevi na vitendo viovu.

Amesema kuwa Serikali haitamvumilia mtu anayeacha majukumu, huku akiwataka kuifanya kazi hiyo kwa weledi na uaminifu mkubwa ili hata mwakani waweze kuteuliwa tena.

Kwa wilaya ya Ngara mkoani Kagera  kwa mwaka 2018  Jumla ya Watainiwa ni 5,095; watafanya Mtihani wa Darasa la saba ulioanza leo September 5 hadi 6,2018 ,Wasichana wakiwa ni 2,644 na Wavulana ni 2,451.

Kati yao Watahiniwa watatu wavulana wawili na msichana mmoja, wana uoni hafifu (Low Vision); ambapo wavulana wanatoka shule ya msingi ya Ruganzo na msichana anatoka katika shule ya msingi ya Muhweza.

Post a Comment

0 Comments