habari Mpya


Watu 9 wakutwa na VVU Sengerema.

Watu 9 Kati ya 725 waliojitokeza kupima Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi katika mkesha wa Mwenge wa Uhuru 2018 katika Halmashauri  ya wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza wamekutwa na maambukizi ya virusi hivyo.


 Akitoa taarifa ya Matokeo ya waliojitokeza kupima afya zao kwa hiyari  baada ya mkesha wa Mwenge wa Uhuru usiku wa kuamkia August 30, 2018 mjini Sengerema, Mkurugenzi  Mtendaji wa Halmashauri hiyo Bw.Magesa Mafuru Bonifas amesema kuwa Wanaume waliojitokeza ni 413 ,walioambukizwa ni wanne na Wanawake waliojitokeza walikuwa 312 na waliokutwa na maambukizi ni Wanawake watano.
 
Bw.Magesa amesema kuwa katika mkesha huo pia watu 300 wamejitokeza kupima ugonjwa wa malaria.

 Mwenge wa Uhuru 2018 sasa unaendelea na mbio zake katika Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema ambapo unaendelea kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi ya maendeleo.

Post a Comment

0 Comments