habari Mpya


Ujenzi Holela Kikwazo Kukabili Majanga ya Moto Mwanza.

Na Maria Philbert -RK Mwanza.

Kutokuzingatia taratibu za ujenzi wa makazi   kwa baadhi ya Wananchi Mkoani Mwanza kumepelekea jeshi la zima moto kushindwa kufika eneo la tukio kwa wakati pale kunapotokea majanga ya mato.
Kauli hiyo imetolewa  na Kaimu  Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mwanza  Agustine Magere akizungumza na redio kwizera na kwamba  jambo hilo linawafanya waonekane hawafiki  kwa wakati maeneo husika  kumbe  chanzo ni wananchi wenyewe. 
Kamanda Magere  amesema  ni vema wananchi  wakafuata utaratibu  wa ujenzi wa makazi  kwa kuwashirikisha watu wa mipango miji ili  kuacha njia  ya kupita gari la zimamoto  pale panapotokea  majanga ya moto.

Wiki ya Zimamoto na Uokoaji kitaifa mwaka huu inafanyika jijini Dodoma ikiwa na kauli mbiu isemayo kuinua uchumi wa viwanda funga vingamua moto kwenye kiwanda chako.

Post a Comment

0 Comments