habari Mpya


Tani 13 za Kahawa ya Magendo yakamatwa Wilayani Misenyi Ikisafirishwa.

Moja ya lori lililokamatwa likitorosha Kahawa.

Na William Mpanju –RK Misenyi.

Serikali wilayani Missenyi mkoani Kagera imekamata tani 7 za kahawa zikisafirishwa kwa njia ya Magendo kwenda katika nchini jirani ya Uganda.

Mkuu wa wilaya ya Missenyi Kanali Denis Mwilla amesema hayo August 30, 2018 wakati akiongea na waandishi wa habari juu kukamatwa kwa kahawa hizo.

Amesema kuwa kahawa hizo zimekatwa usiku katika Kata ya Bwanjai Tarafa ya Kiziba zikiwa zinasafirishwa kwenye Lori lenye namba za usajili T 467 ARL  aina ya Fuso

Amesema baada ya kakamatwa, Mfanyabiashara aliyekuwa anasafirisha kahawa hizo kinyume cha sheria Bw Johakimu Martin amekiri kuwa alikuwa anazipeleka nchini Uganda kupitia mpaka wa nchi ya Tanzania na Uganda wa Kashenye

Kanali Mwilla ameongeza kuwa Serikali imeimalisha ulinzi katika maeneo ya mipaka ili Kudhibiti Magendo ya kahawa na kwamba katika msimu huu wa Mavuno , Serikali Wilayani Missenyi imeshakamata Jumla ya tani 13 za kahawa maganda na tani 8 za kahawa Safi zenye thamani ya shilingi milioni 40.
Pamoja na kukamata kahawa hizo amesema pia jumla ya magari 8 na pikipiki 5 zimekamatwa na watuhumiwa 12 ambao kesi zao ziko Polisi na kuwa taratibu zikikamilika watafikishwa Mahakamani

Hata hivyo Mkuu huyo wa Wilaya ya Misenyi mkoani Kagera ametoa wito kwa Watanzania wazalendo kutoa taarifa za kufichua Magendo ya kahawa na kwamba Serikali imetenga donge nono la fedha kama motisha kwa wale watakaotoa taarifa zitakazosaidia kakamatwa kwa watu wanaofanya biashara ya Magendo ya kahawa.

Post a Comment

0 Comments