habari Mpya


Serikali yaagiza Ma DC Kagera Kujipanga kudhibiti Ebola.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Bi. Ummy Mwalimu  akiwa eneo la Rusumo wilayani Ngara mkoani Kagera pamoja na kutoa maagizo ya namna ya kuukabili Ugonjwa wa Homa ya Ebola kwa tanzania pia alipokea taarifa kutoka kwa Bw.Stanley Chipasula ,Mtoa huduma za Afya katika kituo cha kupima Afya Wageni wanaoingia nchini kupitia mpaka wa Rusumo.
Serikali imewaagiza wakuu wa wilaya za mkoa wa Kagera kutenga Zahanati zitakazopokea na kuwahudumia Wagonjwa wa Homa ya Ebola  endapo watabainika.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Bi. Ummy Mwalimu akiwa ziarani Jana August 27, 2018 katika mpaka wa Tanzania na Rwanda  eneo la Rusumo wilayani Ngara ili kuangalia ni kwa jinsi gani mkoa wa Kagera umejipanga kudhibiti ugonjwa huo.

Waziri Ummy amesema Shirika la Afya Duniani (WHO)  limetoa taarifa mpya ya kwamba Tanzania ipo katika hatari kubwa ya kupata maambukizi ya ugonjwa huo kutokana na mwingiliano wa wasafiri kati ya Tanzania na nchi jirani za Rwanda, Burundi, DRC na Uganda.

Ameagiza Mkoa wa Kagera kuhakikisha unadhibiti wasafiri wote wanaopita mipaka rasmi na wale wanaopita njia za panya hasa kutoka Nchini Burundi ili kuwatambua wahisiwa na watakaobainika wanaugonjwa wa Ebola.
Waziri Ummy Mwalimu akikagua banda maalum kwa ajili ya shughuli zakuwapumzisha  raia wa kigeni  wanaobainika au kuhisiwa kuwa na dalili za ugonjwa Ebola.
Hata hivyo Waziri Amesema Serikali kupitia Wizara ya Afya wameshatoa mafunzo kwa watoa Huduma za Afya jinsi gani ya kuwahudumia watu wanaohisiwa au wenye ugonjwa wa ebola sambamba na utoaji wa vifaa kwa ajili ya kinga na kwamba hadi sasa hakuna mtu ambaye amebainika kuwa na ugonjwa wa ebola hapa nchini Tanzania.

Post a Comment

0 Comments