habari Mpya


RC Kagera -Maafisa Kilimo na Ugani Marufuku Kukaa Ofisini,Ni Wakati wa Kutoa Elimu Kwa Wakulima Mashambani.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Marco E. Gaguti awaagiza Maafisa Kilimo na Maafisa Ugani kutokaa Ofisini bali wakawatembelee kuwafundisha na kutoa elimu ya kilimo chenye tija wakulima katika Mkoa wa Kagera wenye fursa ya kustawisha mazao ya aina mbalimbali na masoko ya mazao hayo yapo ya kutosha.

Gaguti ameyasema hayo hivi karibuni na kwamba  sasa umefika wakati wa Wataalam wa kilimo kuwafuata wakulima na kuwapa elimu katika maeneo yao kuliko wakulima kuwafuata wataalam.

Ninayo taarifa kuwa Kagera tunavyo viwanda vikubwa tisa lakini vinazalisha chini ya kiwango kutokana na kukosa malighafi zinazotakiwa kuzalishwa kutokana na kutopatikana kwa wingi. Sasa umefika wakati wakulima kuachana na kilimo cha mazoea cha kulima ekari kumi na kupata gunia 10 bali mkulima alime ekari moja avune gunia 20 za mazao, pia kuachana na ufugaji wa kufuga ng’ombe kumi na kupata lita 10 za maziwa bali mfugaji afuge ng’ombe mmoja apate lita 20 za maziwa.” Alifafanua  Gaguti.

Mkuu huyo wa Mkoa wa Kagera, alifafanua zaidi kuwa mkoa wa Kagera unayo fursa kubwa zaidi ya kilimo kwani hali ya hewa na ardhi yake inaruhusu kilimo cha zao lolote kwa hiyo wananchi wanatakiwa kuitumia fursa hiyo kuhakikisha wananlima mazao mbalimbali kwa wingi na masoko ya mazo hayo yapo kwakuwa Kagera inapakana na nchi tano ambazo ni fursa ya masoko ya mazao yanayolimwa.


Post a Comment

0 Comments