habari Mpya


Mwanafunzi wa Darasa la 5 Bukoba,Amefariki Baada ya Kupigwa Fimbo na Mwalimu Wake.

Mwanafunzi wa darasa la 5 mwenye umri wa Miaka 13, Spelius Eradius wa shule ya msingi Kibeta iliyoko manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera amefariki baada ya kupigwa fimbo na mwalimu wake.

Akizungumza na vyombo vya habari Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Kagera ulikopokelewa mwili huo Jana August 27,2018 Bw John Mwombeki amesema uchunguzi uliofanyika umebaini kuwa kifo cha mwanafunzi huyo kimetokana na kipigo alichokipata.

Amesema kwa kushirikiana na jeshi la polisi uchunguzi unaendelea huku akiwasihi wazazi, walezi na jamii kuishi vizuri na watoto wao kwani hali ya mtoto huyo haikuwa ya kuridhisha kwani alionekana amekua akiadhibiwa mara kwa mara.


Kwa upande wake mlezi wa mtoto huyo aliyefahamika kwa jina la Justus Balilemwa amesema ameishi na mtoto huyo tangu akiwa mdogo hakuwa na tatizo lolote .

Jeshi la Polisi mkoani Kagera limefika eneo la tukio na linaendelea kushirikiana na madaktali kwa uchunguzi zaidi .

Post a Comment

0 Comments