habari Mpya


Ligi Tanzania Bara 2018/2019 -Simba SC yaanza Vyema kutetea Ubingwa.

Mabingwa watetezi, Simba SC wameanza vyema Ligi Kuu ya Tanzania Bara 2018/2019 baada ya kuichapa Tanzania Prisons ya Mbeya bao 1-0 katika mchezo uliofanyika Usiku Jana August 22, 2018 Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.

Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, mshambuliaji kutoka Rwanda mwenye asili ya Uganda, Meddie Kagere aliyefunga dakika ya pili kwa shuti kali baada ya kupewa pasi nzuri na Nahodha, John Raphael Bocco kutoka upande wa kulia.

Katika mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Ndanda FC walipata ushindi wa ugenini wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Ruvu Shooting Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani, Singida United wamefungwa 1-0 nyumbani Uwanja wa Namfua na Biashara United na Alliance FC pia imefungwa 1-0 na wapinzani wao wa jiji, Mbao FC Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.

Kagera Sugar imeanza vizuri kwa ushindi wa 2-1 nyumbani dhidi ya Mwadui FC Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba na Coastal Union, timu kipenzi cha Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imelazimishwa sare ya 1-1 Lipuli FC Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.
Ligi hiyo inaendelea leo August 23, 2018, Yanga SC wakiwakaribidsha Mtibwa Sugar Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam Saa 12:00 jioni, JKT Tanzania watamenyana na KMC kuanzia Saa 8:00 mchana Uwanja wa Meja Isamuhuyo, Stand United na African Lyon Saa 10:00 Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga na Azam FC na Mbeya City kuanzia Saa 2:00 usiku Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

Post a Comment

0 Comments