habari Mpya


Halmashauri ya Wilaya ya Ngara yatoa Milioni 30 kwa Vikundi vya akina Mama na Vijana.

Bi. Josephine Lusatira.

Idara ya Maendeleo ya Jamii katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara,mkoani Kagera imefanikiwa kukopesha vikundi vya akina Mama na Vijana shilingi milioni 30,000,000/= katika mwaka wa fedha wa 2017/2018.

Kaimu Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Bi. Josephine Lusatira, akiongea na Radio Kwizera  ofisini kwake Agosti 13,2018, amesema Katika mwaka wa fedha wa 2017/2018, makadirio ya makusanyo ya Halmashauri kwa mwaka, yalikuwa shilingi 1,035,005,000/=,  na kutoa asilimia 10% ya T.shs. 103,500,500/= kwa vikundi vya wanawake na vijana.

Makusanyo halisi hadi Juni 30, 2018 ilikuwa T.shs. 930,708,085.20, ambapo asilimia 10% ni T.shs 93,070,808.52 na kwamba Marchi, 2018, walikopesha shilingi 13,621,730/= kwa vikundi 10, vikundi 5 vya vijana vilikopeshwa shilingi 6,810,865.00 na vikundi 5 vya wanawake shilingu 6,810,865.00 sawa na asilimia 16.8%.

Mwishoni mwa mwezi Juni, 2018, idara yake ilikopesha vikundi 8 shilingi 16,378,270/=, ambapo vikundi 2 vya vijana vilipokea shilingi 5,000,000/= na vikundi 6 vya akina mama vilikopeshwa shilingi 11,378,270/=.

Bi. Lusatira amebainisha kuwepo kwa changamoto mbalimbali, ambazo halmashauri ya wilaya ya Ngara inakumbana nazo katika kutoa mikopo kwa vikundi vya vijana na wanawake, ambazo ameainisha kuwa ni ufinyu wa bajeti na makusanyo kidogo ya halmashauri.

Amesema ufinyu huo husababisha idara ya Maendeleo ya Jamii, kushindwa kuvifuatilia vikundi vilivyopewa mikopo, kwa ajili ya kutoa ushauri na kuhamasisha kurejesha mikopo katika muda uliopangwa.

Bi. Lusatira amesema baadhi ya vijana ugawana fedha za mikopo, walizopewa kwa matumizi mengine, na kushindwa kurejesha mikopo kwa wakati, na kwamba baadhi ya wakopaji wanahamia nje ya wilaya, kwaajili ya utafutaji bila kurejesha mikopo waliyochukua.

Idara inaendelea kufanya ufuatiliaji kwa vikundi vya vijana na wanawake, vilivyochelewa kurejesha mikopo waliyopewa ili kuwezesha vikundi vingine kupatiwa mkopo.

Post a Comment

0 Comments