habari Mpya


Dereva afariki ,Magari Saba yakiteketea kwa Moto Wilayani Ngara.

Muonekano wa Magari Saba ya mizigo na Trekta moja yakiwa yameteketea kwa moto katika kituo cha forodha cha Rusumo Wilaya ya Ngara mkoani Kagera mpakani mwa Tanzania na Rwanda baada  ya gari la Mafuta ya petrol kupoteza mfumo wa breki na kuyagonga magari mengine yaliyokuwa yakisubiria utaratibu wa kuvuka mpakani kisha moto kulipuka na kusababisha mengine kupatwa moto huo.

Katika Tukio hilo lililotokeoa leo August 19,2018 majira ya saa 08:45 Asubuhi, Mtu mmoja ameripotiwa kufariki dunia aliyekuwa Dereva kwenye Lori lililosababisha ajali.
Helkopta ya Kikosi cha zima moto toka Nchini Rwanda  kimesaidia kuuzima moto  huo, ambapo kwa mujibu wa mashuhuda waliokuwepo eneo la tukio wamesema kuwa moto ulikuwa mkubwa na kulikuwa na Hatari ya kuteketeza Ofisi za kituo cha forodha,Benki ya NMB na Magari mengineyo huku baadhi ya Wananchi wakijeruhiwa kutokana na kupata taharuki.
Hata hivyo, Mkuu wa wilaya ya Ngara, Luteni Kanali Michael Mtenjele amesema ukosefu wa zimamoto ni changamoto kubwa wilayani Ngara kutokana na matukio ya ajali ya moto kuongezeka na ombi lilishatumwa serikalini lakini utekelezaji wake haujafikiwa.
Mkuu wa wilaya ya Ngara Luteni kanali Michael Mntenjele ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo amesema utingo wa gari hilo alibahatika kuruka na kuumia na amekimbizwa hospitali ya Nyamiaga kwa matibabu.

Wakala wa forodha kituo cha Rusumo Abdul Shakuru amesema gari lililosabanisha ajali ni mali ya kampuni ya Lake Oil na magari mengine ikiwemo kampuni ya Azam ambayo hufanya shughuli zake za kisafirisha mizigo kutoka Tanzania kwenda nchini Rwanda.

Post a Comment

0 Comments