habari Mpya


Azam yaichapa Mbeya City Chamazi, yakaa Kileleni Ligi Kuu.

Azam FC vs Mbeya City kwenye dimba la Chamazi, Dar es Salaam. 

Azam FC imeanza vyema Ligi Kuu ya Tanzania Bara 2018/2019 baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mbeya City usiku wa jana August 23, 2018 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam.

Ushindi huo unaifanya Azam FC iongoze Ligi Kuu sasa baada ya mechi za raundi ya kwanza, kutokana na kupata ushindi mzuri huku magoli ya Azam FC yakifungwa na Joseph Mahundi dakika ya 33 akimalizia pasi ya kichwa ya Danny Lyanga aliyefunga bao la pili dakika ya 45.
Mechi nyingine za Ligi Kuu , Yanga SC imeifunga 2-1 Mtibwa Sugar Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Stand United imeichapa 1-0 African Lyon Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga wakati, KMC imelazimisha sare ya 0-0 na JKT Tanzania Uwanja wa Meja Isamuhuyo, Mbweni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Na August 22, 2018 mabingwa watetezi Simba SC wealishinda 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons Uwanja wa Taifa, Ndanda FC washinda ugenini 1-0 dhidi ya wenyeji, Ruvu Shooting Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani, Singida United walifungwa 1-0 nyumbani Uwanja wa Namfua na Biashara United na Alliance FC pia walifungwa 1-0 na wapinzani wao wa jiji, Mbao FC Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.

Kagera Sugar iIianza vizuri pia kwa ushindi wa 2-1 nyumbani dhidi ya Mwadui FC Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba na Coastal Union, ililazimishwa sare ya 1-1 Lipuli FC Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.

Post a Comment

0 Comments