habari Mpya


Ureno na Argentina Nje Kombe la Dunia 2018 -Leo Hispania na Urusi kuwafata.?

Timu ya Taifa ya Ureno imeungana na Argentina kuyaaga mashindano ya Kombe la Dunia 2018 ikikubali kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Uruguay.

 Leo Jumapili July 01,2018 Hispania watacheza na wenyeji Urusi  (11:00 Jioni) huku Croatia akiwavaa Denmark(3:00 Usiku)

 
Ushindi wa Uruguay umetokana na mshambuliaji wake anaeichezea klabu ya PSG kutoka Ufaransa, Edinson Cavani aliyetupia mabao yote mawili katika dakika ya 7 na 62.

Bao pekee la Ureno limefungwa na Pepe dakika ya 55 kwa njia ya kichwa kupitia mpira wa kona.

Matokeo hayo yanawafanya nyota Cristiano Ronaldo na Lionel Messi wakosekane sasa kwenye michezo ijayo baada ya kuyaaga rasmi mashindano hayo.

Wachezaji Messi na Ronaldo walikuwa wanatazamwa zaidi na wafuasi wao kutokana na ushindani mkubwa pamoja na ushawishi walionao pale wanapohusika katika mashindano yoyote kwa pamoja kutokana na kuwa ,wana mafanikio makubwa ambayo hayajatokana na timu zao za TAIFA Ila ni ya ngazi ya Vilabu na Michezo mingine.

 

Post a Comment

0 Comments