habari Mpya


Serikali za Tanzania Burundi na Rwanda zaridhishwa na ujenzi wa mradi wa umeme wa maporomoko ya Rusumo

Shaaban Ndyamukama, Ngara
Serikali za Tanzania Burundi na Rwanda zimeridhishwa na hatua ya ujenzi wa mradi wa umeme wa maporomoko ya mto Rusumo ulioko wilaya ya Ngara mkoani Kagera unaotarajia kukamilika Februari mwaka 2020

Waziri wa nishati wa Tanzania Dkt Medard Kalemani akiongea baada ya kuzungukia mradi huo akiwa na mawaziri wa wa nishati wa nchi hizo  na kufanya kikao cha ndani amesema mradi huo unajengwa na wakandarasi wa kichina  na utagharimu dola za marekani 468. Kati ya hizo

Dkt Kalemani amesema  mradi huo utagharimu Dola za kimarekani 468 milioni  kati ya hizo dola 340 milioni  zitatumika kuchimba bwawa na dola 128 milioni  kujenga njia za kusafirisha umeme ambao utazalishwa megawatts 80 kwa kila nchi kupata megawatts 27  
Akitoa   ufafanuzi wa mradi  eneo la Rusumo mpakani mwa Tanzania na Rwanda  amesema  miongoni mwa faida zitakazopatikana ni  ajira ya watu 488 katika hatua za awali na mpaka unakamilika utakuwa umetoa wataalamu 100 kila nchi wenye ujuzi wa kuzalisha umeme wa maji.
Alisema umeme huo utachochea kuwepo kwa wawekezaji katika sekta ya viwanda ikiwemo uzalishaji wa madini  ya Nickel kata ya Bugarama hivyo wananchi watumie miradi hiyo kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo kwa ajili ya chakula na biashara.
"Tunatarajia kupokea hata watalii kutokana na eneo hili kuwa lenye kuvutia milima mabonde ambapo mradi huu pia utakuwa na miundombinu inayochochea kuharakisha maendeleo" Alisema Dkt Kalemani
Pia alisema fedha zinazojenga mradi huu zimetolewa na benki ya dunia hivyo kunafanyika ufuatiliaji na usimamizi mkubwa kwa kila nchi kuhakikisha hakuna ubadhilifu na wakandarasi watakaofanya hujuma hatua kali zitachukuliwa.
Mbunge wa jimbo la ngara Alex Gashaza alisema serikali haina budi kuweka njia mbadala ya kusaidia wananchi kuvuka mto Ruvubu ambapo kivuko kilichopo hakitumiki baafa ya kujaa   maji na kusababisha kisifanye kazi.

Alisema Kivuko hicho kimedumu bila kuhudumia wananchi miezi miwili sasa na wananchi wanstumia mitumbwi kuvuka kitoka kijiji upande mmoja kwenda mwingine na kwa gharama kubwa kiasi cha Sh4000 kwenda na kurudi
Alisema mitumbwi inayotumika haina usalama kwa maisha ya abiria lakini mashamba ya wananchi yenye mazao mbalimbalo na baadhi ya  makazi yao yamezingirwa na maji  hivyo licha ya mradi kuwa na manufaa athari hizo zitafutiwe ifumbuzi
"Watu wengi hususan wakazi wa Ngara watafaidika na miradi ya kijamii itakayojengwa kama kituo cha Afya katika kijiji cha Rusumo , miradi ya maji  katika vijiji vitano vya kata hiyo yenye thamani ya Sh200 milioni" Alisema Gashaza.
Waziri wa nishati nchini Rwanda balozi Clavery Gatete ameshukuru mahusiano yaliyopo baina ya nchi tatu zitakazonufaika na mradi huo kwa kushirikishana na kufuatilia kila hatua kwa pamoja kushauriana na wakandarasi ili zipatikane fursa za kuinua uchumi wa wananchi
Amesema baada ya mradi kukamilika kila nchi na jumuia ya Afrika mashariki na kati itakuwa na maendeleo kutokana na mwingiliano wa kibiashara katika uzalishaji Mali zikuwemo bidhaa zinazohitajika kuongeza uzalishaji wa viwanda.
"Nikiwa mwenyekiti ambaye nimemaliza muda wangu katika usimamizi na ufuatiliaji wa mradi huu ninategemea mwenzangu wa Tanzania atazingatia ushauri wetu na wataalamu kuhakikisha unakamilika kwa viwango vyenye ubora" Alisema Gatete
Katika ziara ya mawaziri hao kukagua ujenzi wa mradi wa umeme katika maporomoko ya Rusumo pia amechaguliwa Dkt Medard Kalemani kuwa Mwenyekiti wa mawaziri wa nishati wa Tanzania, Rwanda na Burundi kwa kipindi cha mradi unavyoendelea kujengwa.

Post a Comment

0 Comments