habari Mpya


Serikali yaagiza Viongozi KCU na KDCU Kagera Kuchunguzwa.

Naibu waziri wa Kilimo Bw. Omary Tebweta Mgumba ameagiza tume ya taifa iliyochunguza bodi ya Korosho na Tumbaku ishirikiane na vyombo vya uilinzi na usalama mkoani Kagera ichunguze viongozi wa vyama vikuu vya ushirika vya ununuzi wa kahawa mkoani Kagera kwa makosa mbali mbali ikiwemo kulipa deni la zaidi ya shilingi bilioni 4 kwenye benk ya CRDB badala ya kulipa wakulima. 

Bw. Mgumba amesema hayo wakati akizungumza na wakulima wa zao la kahawa kwenye mkutano wa hadhara ulifanyikia katika kata ya Birabo wilayani Muleba mkoani Kagera baada ya wakulima kulalamikia bei ya kahawa na kutolipwa fedha zao zaidi ya miezi miwili.
 
Amesema kuwa pamoja na kuagiza viongozi hao wa vyama vikuu vya ushirika KCU na KDCU Kukamatwa bado wanatakiwa kuchunguzwa kwa makosa ya kuhujumu uchumi ikiwemo bei ya awali ya kahawa badala ya kuwa 1,460 inanunuliwa shilingi 1,000.
 
 
Kwa upande wao baadhi ya wakulima waliokuwa kwenye mkutano huo wamesema kuwa pamoja na kuchukuliwa hatua viongozi hao wameiomba Serikali kuagalia upya utaratibu wa kuuza kahawa kwenye vyama vya ushirika kutokana vyama hivyo havina fedha za kutosha za kununua kahawa kutoka kwa walima hao.

Post a Comment

0 Comments