habari Mpya


Prof.Anna Tibaijuka:Viongozi wa Vijiji na Kata toeni elimu kwa wakulima wa zao la kahawa juu ya usafirishaji wa zao hilo.

Muleba na Shafiru Yusufu
Mbunge wa jimbo la Muleba Kusini profesa Anna Tibaijuka amewataka
viongozi wa vijiji na Kata wilayani Muleba mkoani kagera  kuwapatia elimu juu ya usafirishaji wa kahawa  kabla hawajawachukulia hatua za kisheria
Akiongea kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika  July 9 mwaka huu katika kata ya Muleba wilayani humo baada ya wananchi wa kata hiyo kulalamikia viongozi wa kata hiyo kuwakamata wakiwa wanasafirisha Kahawa zao Kutoka shambani kuelekea nyumbani.

Kwa upande wake Afisa kilimo wilaya ya Muleba Bw. Charles Mayunga
amesema kuwa utaratibu uliopo mkulima haruhusiwi kusafirisha kahawa
zake kwenye chombo cha usafiri ambacho kipo wazi hivyo lengo la
maafisa ugani wakishirikiana na kamati za ulinzi na usalama wa kijiji
na kata ni kuhakikisha mkulima hasafirishi kwenye usafiri wa aina hiyo
ili waweze kuuzaa kahawa iliyo safi.

Nao baadhi ya wakulima waliokuwa kwenye mkutano huo wamesema kuwa wamekuwa hawana uhuru wa zao hilo kutoka na utaratibu mpya uliowekwa na serikali.


Post a Comment

0 Comments