habari Mpya


Nditiye azitaka Kampuni za Simu kutoa Huduma ya Data kwenye Vijiji Nchini.

 
Wanakiji wa kijiji cha Mkulula kilichopo Kata ya Malenga Makali mkoani Iringa wakimsikiliza Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (hayupo pichani) kuhusu jitihada za Serikali za kuwapatia wananchi mawasiliano wakati wa ziara ya Kamati ya Bunge ya Miundombinu kwenye kijiji hicho ya ukagua upatikanaji wa mawasiliano.


Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Amina Masenza (wa kwanza kulia) ramani ya maeneo yanayopata mawasiliano mkoani humo wakati wa ziara ya Kamati ya Bunge ya Miundombinu ya kukagua upatikanaji wa mawasiliano kwenye mkoa huo. Anayeshuhudia katikati ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Hawa Mchafu.

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kushoto) akiteremka kwenye kilima kilichojengwa mnara wa mawasiliano wakati wa ziara ya Kamati ya Bunge ya Miundombinu ya kukagua upatikanaji wa mawasiliano kwenye kijiji cha Mkulula kilichopo Kata ya Malenga Makali mkoani Iringa. Wa pili kulia ni mjumbe wa Kamati hiyo Mhe. Bhagwanji Meisuria.


Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeyataka makampuni ya simu nchini kutoa huduma za data kwa wananchi waishio vijijini na maeneo yasiyo na mvuto wa kibiashara ambapo makampuni hayo yamejenga minara kwa ajlii ya kuwapatia wananchi mawasiliano.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Ndiye wakati wa ziara ya Kamati ya Bunge ya Miundombinu ya kukagua upatikanaji wa huduma za mawasiliano kwa wananchi waishio viijijini na maeneo yasiyo na mvuto wa kibiashara wakati akizungumza na wanakijiji wa kijiji cha Mkulula kilichopo Kata ya Malenga Makali mkoani Iringa.

Nditiye amefafanua kuwa kampuni za simu zinatoa huduma ya sauti tu yaani 2G kwenye minara ya mawasiliano waliyojenga badala ya kutoa huduma ya data kwenye maeneo hayo ili wananchi wapate huduma ya intaneti. Amesema kuwa Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) inatoa ruzuku kwa makampuni hizo ili wajenge minara. 

Tunataka wananchi wapate mawasiliano kwa kuwa wanalipia na ni haki yao  ya msingi kuwasiliana na hii ndio Serikali ya Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuhudumia wananchi wa hali zote,” amesema Nditiye.
 
Ameongeza kuwa hadi sasa UCSAF imetoa ruzuku kwa makampuni ya simu ambapo jumla ya kata 530 zimepatiwa huduma ya mawasiliano kwenye maeneo mbali mbali nchini na ujenzi wa mnara mmoja una gharimu kati ya kiasi cha shilingi milioni mia mbili hadi milioni mia tatu.

Akiwa katika ziara hiyo, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Hawa Mchafu amesema kuwa makampuni ya simu yanapowekeza yasiwekeze kwa mahitaji ya kipindi kifupi bali miundombinu ya mawasiliano wanayojenga izingatie mahitaji ya muda mrefu kwa kuwa wananchi wanaongezeka kwenye maeneo hayo na wanakuwa wengi mathalani kwenye eneo la kata hiyo wananchi wananchi wanafanya shughuli za uchimbaji wa madini, kilimo na ufugaji wa samaki. 

Ameongeza kuwa watoa huduma waweke mawasiliano ya data yaani 4G ili wananchi wapate huduma. “Haiwezekani fedha imetolewa na Serikali ya kujenga mnara kiasi cha shilingi milioni 260 halafu wananchi hawawasiliani,” Mhe. Mchafu amesema. 

Amefafanua kwa wanakijiji hao kwa kusema kuwa, “mnara mnauona umejengwa na TIGO kwa kupatiwa ruzuku na Serikali kupitia UCSAF kiasi cha shilingi milioni 260, nawaomba muiamini Serikali kuwa itatua kero zenu” Mhe. Mchafu amesema.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
  

Post a Comment

0 Comments