![]() |
Katika hatua nyingine amewahimiza wanandoa katika familia
kuwa na moyo wa kuhurumiana wakioneshana upendo ambapo wanaume wajihadhari na
vitendo vya kuwapiga wake zao kwa mateke mithili ya anayewasha pikipiki na
kwamba vitendo vya uongo, uchonganishi,umbea havitahili hats mbele za Mungu.
"Baadhi yetu kutoka kanisa katoliki tunakuwa na umbea
kwa maaskofu juu ya matendo ya mapadre, watawa, na hata wanafamilia
wakituhumianana kwa uasherati au uzinzi janani sote ni binadamu hakuna
mkamilifu"Amesema Padre Kempanju.
|
![]() |
Mahubiri ya Paroko
huyo kwenye msiba yamewaondolea simamzi na huzuni ghafla kwa kucheka kufurahia alichowahusia
kutokana na kuchanganya lugha ya kiswahili na kihaya huku akitafrisi kwa
wasiofahamu lugha hizo.
|
![]() |
Mama yake
Brother Deus Byebariro aliyeitwa Imelda Byebariro Rugomora amefariki akiwa na
umri wa miaka 76 akiacha watoto wanane kati ya 11 aliojaliwa kuwazaa ambapo wajukuu ni 28 na vitukuu watatu
akitokea familia ya Chifu Rugomola wa Maruku mkoani Kagera
|
![]() |
Mazishi yake
yaliongozwa na Padre huyo Kempanju ,Padre Damas Missanga, kutoka Radio Kwizera
Ngara na padre Pascal Mwijage chini ya kwaya ya kikatoliki kutoka kigango cha
Kahororo na waumini wa madhehebu mbalimbali ya kidini kutoka maeneo mbalimbali
vikiwemo vyombo vya ulinzi na usalama
|
![]() |
Pichani ni sehem ya watu walio hudhuria katika idaaba ya Mazishi. |
![]() |
Pichani wa kwanza kushoto ni Brother Deusdedith Byebarilo Muhasibu wa Radio kwizera aliye fiwa na Mama yake Mzazi na pembeni yake ni Afisa masoko wa Radio kwizera Donatus Bartazari wakiteta jambo |
![]() |
Pichani ni Baadhi ya Wafanyakazi wa Radio kwizera walio fika kumfariji Br.Deus Brother Deusdedith ni Bruda kutoka shirika la watawa wanaume wa katoliki wa marafiki wa Yesu {Jesuit Fathers}. |
0 Comments