habari Mpya


Msaidieni Bi.Salaiya Selemani wa Mtaa Buyekera – Bakoba.

Bi.Salaiya Selemani ni mkazi wa mtaa Buyekera Kata Bakoba Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera, anaishi kwenye Kibanda ( PICHANI )alichojengewa baada ya nyumba aliyokuwa akiishi kuangushwa na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani humo September 10,2016.

Bibi huyu  anaishi na wajukuu zake wa 3 na amekuwa akihangaika kuwatafutia chakula wajukuu zake kwa kufanya kazi za vibarua kwenye makazi ya watu.

Anaililia Serikali , Wadau na Jamii kumsaidia japo akajengewa Nyumba yenye chumba kimoja na mtu wa kuwanunulia sare na vifaa vya shule Wajukuu zake ili wapate kusoma.

Na- Anord Kailembo –RK Bukoba.

Post a Comment

0 Comments