habari Mpya


Mkulima Ngara atakayeuza Kahawa bila kufata Utaratibu wa Serikali ,Kuchukuliwa hatua.

Chama cha ushirika Wilayani Ngara Mkoani Kagera Ngara Farmers kimetengewa Jumla ya kiasi cha shilingi Bilioni 1 na milioni 226 kwa ajili ya ununuzi wa zao la kahawa.

Kauli hiyo imetolewa na Afisa kilimo Wilaya ya Ngara Bw Costantine Mdende akiwataka Watendaji wa Vijiji na Kata kusimamia na kuwaelimisha wananchi juu ya maelekezo yaliyo tolewa na Serikali kuhusu  utaratibu unao takiwa wakati wa ununuzi na uuzaji wazao  hilo.
Aidha Bw.Mdende ameongeza kuwa Mwananchi yeyote atakaye uza kahawa yake bila kuzingatia maelezo yaliyo tolewa na Serikali   hatua kali za kisheria zita chukuliwa dhidi yake ikiwemo kwa mtu Binafsi faini yake ni kuanzia milioni 10, Kampuni ni kuanzia milioni 100 sambamba na Kifungo.

Wakizungumza na Radio Kwizera baadhi ya Watendaji wameahidi kuyazingatia Maelekezo waliyopewa  huku wakisema wana kwenda kuwaelimisha wananchi juu ya madhara yanayo weza kujitokeza endapo watauza kahawa bila kuzingatia maelekezo ya Serikali.  

Post a Comment

0 Comments