habari Mpya


Mbunge Kahama –Ashangazwa kutokamilika Shule ya Sekondari Busoka iliyojengwa Miaka 10.

Muonekano wa Shule ya Sekondari Busoka iliyopo Kata ya Busoka wilayani Kahama mkoani Shinyanga iliyojengwa miaka 10 iliyopita na mpaka sasa haijafunguliwa na imeanza kupukutika kabla ya kutumika.

Habari/Picha –Simon Dioniz –Rk Kahama.

Akitembelea Shule hiyo katika ziara yake,Mbunge wa Jimbo la Kahama mjini mkoani Shinyanga Bw. Jumanne Kishimba amewataka wakazi wa Kata hiyo ya Busoka kuhakikisha wanatoa ushirikiano ili kuweza kukamilisha shule yao ya sekondari Busoka ambayo imeshindwa kukamilika kwa zaidi ya miaka 10

Akizungumza na wakazi wa kijiji cha Kitwana Mbunge Kishimba amesema kuwa ikiwa wananchi watashirikiana shule hiyo itakamilika ikiwemo na nyumba ya mwalimu ambayo imeishia kwenye Madirisha na yeye amechangia shilingi laki 5.

 
Amesema kuwa tayari wamekubaliana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji kuhakikisha Wanakarabati Majengo hayo na Wanafunzi waweze kupokelewa kuanzia mwakani 2019, kwani kwa sasa Wanafunzi wa Kata hiyo hutembea zaidi ya kilomita10 kwenda shule ya Baba Haji Sekondari.

Wananchi wa kata ya Busoka, wameanza ujenzi wake mwaka 2003 ambapo madarasa ya shule hiyo yameshakuwa chakavu kabla ya kutumika na vyumba vutano vya madarasa vimekamilika isipokuwa hakuna nyumba ya mwalimu.

Post a Comment

0 Comments