habari Mpya


Madiwani Misenyi wamcharukia DED kuhusu Hoja za CAG Zilizokosa Majibu.

Na-Wiliam Mpanju Rk Misenyi. 

Baraza la Madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Missenyi mkoani Kagera limesema hawajaridhishwa na majibu ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Bw.Limbe Benard juu ya majibu ya hoja za mkaguzi wa hesabu za serikali CAG ambazo zilikosa majibu kwa miaka mitano iliyopita.

 Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya missenyi Bw. Projestus Tegamaisho amesema hayo katika kikao maalum cha baraza la madiwani kilichoketi kwa ajili ya kujadili hoja za mkaguzi wa hesabu za serikali CAG zilizokosa majibu katika miaka mitano mfululizo kuanzi 2011 hadi 2017 ambapo Mkuu wa Mkoa wa Kagera  aliagiza hoja hizo zitafutiwe majibu.
Amesema majibu ya Mkurugenzi juu ya hoja hizo ni ya ubabaishaji nakumtaka ajipange kuhakikisha anakamilisha majibu ya hojat hizo vinginevyo watamwazimia ili kumchukulia hatua kwa kushindwa kuwasimamia watendaji wake na kusababisha fedha za serikali kupotea na kuzibadilishia matumizi kinyume cha sheria ikiwemo fedha za mfuko wa vijana na wanawake zaidi  ya milioni 79.9 ambazo ni asilimia 10 na hazikutolewa na halamshuri kwa mujibu wa sheria. 
Nao baadhi ya Madiwani wamemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bw.Limbe Benard  kuwa makini na watalamu wake wanaosimamia fedha ili kuepuka kujibu hoja zisizo za lazima na kuunga mkono hoja ya Mwenyekiti ya kumtaka Mkurugenzi kuwajibishwa pindi  zitakapojitokeza changamoto kama hizo za upotevu wa mali za halimahauri.

 Kwa upande wake Mkurugezi wa halmashauri ya wilaya ya Missenyi amesema amepokea changamoto hiyo na kwamba anendelea kufuatilia baadhi ya viambatanisho vilivyotajwa kwa hoja za mkaguzi na kuahidi kurejesha fedha zaidi ya shilingi milioni 183.722 ambazo zilikopwa kwenye akaunti ya amana huku akiahidi kuendelea kusimamia fedha za serikali na mapato ya halmashauri.

Post a Comment

0 Comments