habari Mpya


Kombe la Dunia 2018: Ni Uingereza dhidi ya Sweden Robo Fainali .

Baada ya kungoja zaidi ya dakika 120, hatimaye, timu ya mwisho kufuzu robo fainali Urusi 2018, imefahamika. 

Uingereza ilitangulia kwa bao la Harry Kane dakika ya 57 kwa penati baada ya yeye mwenyewe kuchezewa rafu na Carlos Sanchez, lakini Yerry Mina akaisawazishia Colombia dakika ta tatu ya muda wa nyongeza baada ya dakika ya 90.

 
Kipa wa Uingereza, Jordan Pickford akichupa kuokoa mkwaju wa penalti wa Carlos Bacca wa Colombia na kuipa timu yake ushindi wa penati 4-3 baada ya sare ya 1-1 ndani ya dakika 120 katika mchezo wa hatua ya 16 Bora Kombe la Dunia usiku wa Jumanne July 3, 2018 Uwanja wa Otkrytiye Arena mjini Moscow, Urusi na sasa itakutana na Sweden katika Robo Fainali. 

 
Uingereza imeondoa nuksi ya kutemwa kwa njia ya matuta na kutua robo fainali kwa mara ya kwanza tangu 2006. 

Wakati huo huo, Uingereza imeshinda mechi ya Kombe la Dunia kwa njia ya penalti kwa mara ya kwanza (3-4).

Waliofunga Uingereza:

  • Kieran Trippier
  • Harry Kane
  • Marcus Rashford
  • Eric Dier
Waliofunga Colombia.
  • Juan Cuadrado
  • Falcao
  • Luis Muriel
Uingereza itatoana jasho na Sweden iliyoifunga Uswisi bao 1-0 , Jumamosi 7/7/2018.

 

Post a Comment

0 Comments