habari Mpya


Fainali Kombe la Dunia 2018 -Croatia na Ufaransa Jumapili July 15.

Timu ya Taifa ya Croatia imefanikiwa kuingia hatua ya fainali ya michuano ya Kombe la Dunia 2018 baada ya kuishushia kipigo cha mabao 2 – 1 Uingereza usiku wa Jumatano July 11, 2018  kwenye Uwanja wa Luzhniki mjini Moscow, Urusi.

Kwa matokeo hayo, Croatia sasa atacheza fainali yao ya kwanza Kombe la Dunia dhidi ya Ufaransa, huku Uingereza wenyewe wakicheza na timu ya taifa Ubelgiji katika mchezo wa kumtafuta mshindi wa tatu.
Mchezo huo uliyokwenda hadi dakika 120 baada ya kumalizika dakika 90 kwa sare ya 1 – 1 imemshuhudia mchezaji Mario Mandzukic akiibuka shujaa kwakuifungia bao la pili na la ushindi timu yake ya Taifa ya Croatia dakika ya 109.
Bao la Uingereza, lilifungwa na Kieran Trippier akifunga dakika ya 5 tu ya kipindi cha kwanza kisha Croatia ikisawazisha kupitia kwa Perisic dakika ya 68 na  kuufanya mchezo huo kuwa mgumu baada ya kumalizika dakika 90 kwa sare hiyo ya 1 – 1.

Croatia sasa itakutana na Ufaransa Jumapili July 15, 2018 katika Fainali ya Kombe la Dunia 2018.

Post a Comment

0 Comments