habari Mpya


DMO NGARA : Wazazi na walezi changieni chakula ili watoto wale shuleni kabla ya kumeza dawa za minyoo tumbo na kichocho.

Ngara na Shaaban Ndyamukama RK.
Wazazi na walezi katika Hamashauri ya Wilaya ya Ngara mkoani kagera , wametakiwa kuchangia chakula kitakachotumika siku ya ugawaji wa dawa za minyoo na kichoho katika zoezi ambalo limeanza leo katika shule za msingi wilyani humo

Mganga mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Dkt. Revocatus Ndyekobora alisema hayo hjana kwa walimu wakuu a wlimu wa afya wilayani humo wakati akitoa mafunzo elekezi ya ugawaji wa dawa za minyoo na kichocho na kwamba walimu wasimamie zoezi la kugawa cakula shuleni wala sio wazazi kule majumbani
Pichani ni Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Buhororo wilayani Ngara Masumbuko bwile akitoa maelezo kwa wazazi kuhusu utaratibu wa utoaji dawa za minyoo kwa watoto.
Aliwataka wazazi wachangie chakula cha kutosha na kiandaliwe shuleni, ili watoto hao waweze kula chakula hicho chini ya usimamizi wa walimu watakaohakikisha kila mtoto atakayepata dawa hizo hakuna madhara yatakayojitokeza.
“Wazazi na walimu mhakikishe watoto wote wenye umri kati ya miaka 05 – 14, wanahudhuria bila kukosa shuleni, ili waweze kupata dawa za kuwatibu magonjwa ya minyoo pamoja na kichocho.” Alisema Dkt. Ndyekobora.
 Picha ni ni wanafunzi wa shule ya msingi Buhororo wakimenya vyakula vya aina mbalimbali na kupika kwa ajili ya kupata  dawa za minyoo na kichocho hii leo
Aidha, alifafanua kwamba dawa za minyoo zitamezwa asubuhi,  kabla ya kupata chai au chakula chochote; huku dawa za kuzuia kichocho watazimiza baada ya kula na kushiba na kwamba chakula hicho kiweni ni kile kinacotumika kwenye familia.
Alisema idara ya Afya imevuka lengo la kitaifa mwaka 2017, kwani ililenga kutoa dawa kwa watoto 79, 156 wakaandikishwa watoto 77,869 na kufanikiwa kuwafikia watoto 68,584 sawa na asilimia 86.2  mwaka 2018 wamelenga   watoto zaidi ya 80,000.

Naye Mganga mfawidhi wa zahanati ya Buhororo  Afya Codratus Mutabihirwa alisema kichocho ni maradhi yanayotokana na  minyoo aina ya schistosomiasis  ambayo hupatikana kwenye maji yaliyotuama  kwenye madimbwi na maeneo mengine katika Mazingira ya  binadamu
 “Ugonjwa huu huwashambulia watu wanaoogelea kwenye madimbwi hayo au kuyanywa na mara nyingi hupitia kwenye ngozi ya mwili au matundu ya ngozi na kusababisha  aidha kichocho cha tumbo au kichocho cha mkojo” Alisema.

Wanafunzi wakifurahia kupata taarifa za kupewa chakula shuleni katika zoezi la kumeza dawa za minyoo na kichocho

Alizitaja dalili za kichocho cha tumbo  ni kuuumwa tumbo kwa kukata ndani na kusikia maumivu , kuharisha kinyesi kilichochanganyika na damu, ambapo  kichocho cha mkojo dalili kubwa ni kuumia wakati wa kukojoa, kutoa damu kwenye mkojo wa mwisho.

Hata hivyo, Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara Aidan Bahama   aliiomba serikali kutafuta utaratibu wa kutoa dawa hizo kwa watoto pasipo kutegemea wafadhili, kutokana na kuwepo mchakato mkubwa wa utoaji fedha kupitia serikalini.
Pia alisisitiza walimu kuwaelimisha wazazi kuhusu umuhimu wa kuchangia chakula kwa wanafunzi watakaomeza dawa hizo kwa sababu  wakizitumia bila mlo huo wanaweza kupata madhara kwa kupatwa na kizunguzungu au kutapika au mwili kuishiwa nguvu.
 
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Buhororo wilayani Ngara Masumbuko bwile akitoa maelezo kwa wazazi kuhusu utaratibu wa utoaji dawa za minyoo kwa watoto

Post a Comment

0 Comments