habari Mpya


AFARIKI BAADA YA KUTUMBUKIA KATIKA BWAWA LA MAJI MKOANI GEITA


GEITA:NA GIBSON MIKA
Kijana mwenye umri wa miaka 20 Mkazi wa kata ya Nyankumbu Mkoani Geita amepoteza maisha baada ya kuzama ndani ya Bwawa la maji  wakati alipokuwa akifuata samaki ng’ambo ya pili ya Bwawa hilo.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Geita  Mponjori Mwabulambo amesema tukio hilo limetokea julai 6 mwaka huu majira ya saa nne asubuhi baada ya kijana huyo kufika katika Bwawa hilo (maarufu kama Bwawa la Mzungu)  kwa lengo la kununua samaki. Pia ameongeza kuwa   baada ya kufika kwa kijana huyo alikuta wavuvi wanaovua samaki wapo ng’ambo ya pili ndipo kijana huyo  alichukua mtumbwi uliokuwa karibu yake na kuanza kuwafuata wavuvi  hao kwa lengo la kununua samaki kutoka kwao na alipofika katikati mtumbwi ulijaa maji kutokana na tundu lililokuwepo kwenye mtumbwi huo yeye bila kutambua.
Pichani juu ni Baba mzazi wa marehem Makoye Misalaba akizungumza na mwandishi wetu. Nae baba wa mzazi kijana huyo Makoye Misalaba amesema kijana wake hakuwa na migogoro,  wala madeni, katika jamii inayowazunguka hivyo kuiomba  jamii kumuombea kwa mwenyezi mungu ili apumzike salama.   
 Hata hivyo,Marehemu ametabulika kwa jina la Yohana Makoye,baada ya mwili     wake kuibuka nakuelea juu maji tangu alipozama.


Hata hivyo baadhi ya wakazi wa kata hiyo waliofika katika eneo la tukio wameiomba serikali kuwasaidia kuvyeka majani yaliyondani ya bwawa ili kuwasadia  kuona shughuli zinazokuwa zinaendelea ndani ya bwawa na kuweza kutoa msada pale unapohitajika kwa wavuvi hao.
Post a Comment

0 Comments