habari Mpya


Wananchi Kigoma –‘’ Madereva Wazembe Barabarani Wachukuliwe Hatua’’.

Na-Adrian Eustas Radio Kwizera –Kigoma.

Wananchi Mkoani Kigoma wamelitaka jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani kuchukua hatua za kisheria kwa kuwafikisha mahakamani Madereva na watu wote wasio zingatia sheria za usalama barabarani.

Kauli hiyo imekuja kufuatia ajali katika eneo la Gungu manispaa ya Kigoma ujiji kutokana na uzembe wa dereva wa basi hilo ambae hakuchukua tahadhari wakati akivuka eneo la reli. 

Katika hatua nyingine Wananchi hao wamesema uwepo wa baadhi ya Askari Polisi wa usalama barabarani wanaojihusisha na vitendo vya rushwa wakati wakitimiza majukumu yao wamekua chanzo kikubwa cha ajali.

Kwa upande wake Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Kigoma ASP Martin Otieno amesema Jeshi hilo halitawavumilia  baadhi ya Madereva wanaokiuka sheria za usalama barabarani ikiwa ni pamoja na kufanya uchunguzi juu ya tuhuma za baadhi ya Askari Polisi wanaojihusisha na vitendo vya rushwa. 

June 6,2018 ilitokea  ajali na Watu 10  kufariki dunia  na wengine 35 kujeruhiwa kufuatia Basi namba T 885 DLD la Prince Hamida lililokuwa likitoka Kigoma kuelekea Tabora kugonga na treni ya mizigo mkoani Kigoma katika eneo la makutano ya barabara na reli eneo la Gungu katika Manispaa ya Kigoma Ujiji.

Basi hilo la Prince Hamida hufanya safari zake kati ya Mikoa ya Kigoma na Tabora.

Post a Comment

0 Comments