habari Mpya


Wakulima Kagera -''Vuneni Kahawa yenu kwa Weledi ili iwe Bora Sokoni''.


Umera Vedasto (48) mkazi wa kitongoji cha Muzinga kijiji na kata ya Nshamba wilayani Muleba mkoani Kagera akivuna kahawa Jana June 29,2018 ndani ya shamba lake.

 Shaaban Ndyamukama RK-Muleba.

Serikali kupitia Wizara ya Kilimo na Ushirika imewataka wakulima wa zao la kahawa kulivuna kwa weledi mkubwa wakitumia vifaa maalumu vya kuvunia na kuianika ili iweze kuwa na ubora katika soko kibiashara.

 Waziri wa kilimo Charles Tizeba amesisitiza zao hilo kutoanikwa chini ya udongo na kuvunwa likiwa limekomaa ili baada ya kupelekwa kwenye minada wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro lisikutwe na takataka au mawe na mchanga.
 
 
Aliagiza vyama vya ushirika kufuatilia maagizo hayo ambapo maafisa kilimo ngazi za vijiji wanadai atakayevuna kahawa nakuianika chini atatozwa faini ya shilingi Milioni nane au kifungo miezi sita.

 "Himizeni wakulima wasivune au kuuza kahawa ambayo ni butura ikiwa changa mashambani kwa sababu kufanya hivyo kunapunguza ubora katika soko la dinia" Alisema Tizeba.

Hata hivyo wakulima wanalalamikia utaratibu huo kitokana na bei kutoeleweka ukilinganisha na gharama zinazotumika katika uvunaji Wakazi wa Nshamba wilayani Muleba mkoani Kagera wamesema wameendelea kuwa na umaskini kwa kukosa soko la kahawa kwani wamezuiwa kuiuza kwa watu binafsi au makampuni.
 
Bi.Alibina Deus (48) naye akisaidiana na wifi yake katika uvunaji kahawa akiokota zilizodondokea kwenye makuti ya Migomba.

Post a Comment

0 Comments