habari Mpya


Wakala wa Barabara TANROAD aanza kuziba mashimo ya Barabara ya Murugarama -Rulenge wilayani Ngara.

NGARA na Shaaban Ndyamukama
Wakati mashimo yakizidi kuongezeka katika barabara ya Nyakanazi Lusahunga mpaka Nyabugombe wilayani Biharamulo wakala wa barabara kuu nchini Tanroad wameanza kuziba mashimo yaliyoko barabara ya Murugarama  mpaka Rulenge wilayani Ngara mkoani kagera

Barabara hiyo yanakozibwa mashimo hayo ni katika kipande cha lami cha daraja la Kumwendo kuelekea Rulenge ama Jululigwa na hiyo lami ilijengwa tangia mwaka 1980 lilipoanza kutumika daraja hilo badala ya kivuko cha kuvuta kwa kamba kuvusha abiria na mizigo

Pamoja na jitihada hizo ambazo hufanyika kukiwa na viashiria vya kupita kiongozi wa kitaifa ni bora Tanroad ikatengeneza kwa kiwango bora cha lami katika barabara kuu ya Nyakanazi Lusahunga mpaka Nyabugombe wilayani Biharamulo

Magari yanayopita eneo hilo yanamilikiwa na wafanyabiashara wanaosafirisha mali katika nchi za Afrika Mashariki na kati ambao wanaolipa kodi serikalini baada ya mali zao kufika bandari ya Dar es Salaam

Barabara hiyo inakuza uchumi wa taifa, lakini pia ukarabati usiwe wa kutengeneza kwa kulunda udongo, na kuweka lami juu maana magari yanayopita yanakuwa na uzito mkibwa kiasi kwamba viraka visivyo imara hubanduka ndani ya muda mfupi hivyo itumike saruji na kokoto sio changarawe kama tunavyokuta wafanyakazi  wakitekeleza majukumu yao katika barabara hiyo.


Hata hivyo akizungumza kupitia kipindi cha sauti ya Jamii kinacho rushwa hapa Radio kwizera fm Meneja wa wa Tanroad mkoa wa Kagera Mhandisi Kasamwa alisema kuhusu hiyo barabara ya Nyakanazi hadi Rusumo itajengwa upya nakwamba kupitia bajeti ya mwaka huu kuna fungu limetengwa kwa ajili ya matengenezo kwani barabara hiyo ina miaka 30 sasa.
Amesema walikuwa wanaziba mashimo ili kupunguza kero ya Magari kuharibika pamoja na ajali lakini pia naibu Waziri wa ujenzi Mhandisi Elias Kwandikwa alisema mwaka huu matengenezo yataanza ikiwa ni pamoja na yeye kufanya ziara kukagua barabarani hizo.
 

Post a Comment

0 Comments