habari Mpya


WAFANYAKAZI ZAIDI YA 5,000 WA MGODI WA DHAHABU CHIBUMBE WATEMESHWA KIBARUA.

GEITA NA GIBSON MIKA
Zaidi ya wafanyakazi Elfu tano waliokuwa wakifanya kazi katika Mgodi wa dhahabu wa Chibumbe Kata ya  Mgusu Wilaya ya Geita wamekosa ajira zao baada ya serikali ya mkoa huo kuwafukuza katika eneo hilo kwa madai kuwa eneohilo linamilikiwa na Mgodi wa dhahabu wa Geita Gold Mine (GGM).

Akizungumza na wafanyakazi wa Mgodi huo  Afisa madini wa Mkoa wa Geita Ally Saidi Ally amewataka wafanyakazi hao kusimamisha shughuli zote zilizokuwa  zikiendelea na  kuondoka katika eneo hilo ndani ya masaa 24 ili kupisha uongozi wa Mgodi wa  Dhahabu (GGM) kuendeleza shughuli zake katika eneo hilo.

Hata Hivyo, wafanyakazi hao wameiomba serikali kuwasaidia kutatua mgogoro huo, kutokana na kile walichoeleza kuwa wamekuwa wakifanya kazi katika mgodi huo kwa muda mrefu na kujipatia kipato kupitia shughuli mbalimbali zinazofanyika ndani ya Mgodi.

Mkuu wa wilaya ya Geita Mwl, helmarn Kapufi wakati akisoma makubaliano yaliyofikiwa katika kujadili mgogoro huo na  pande zote mbili mbele ya kamati ya ulinzi na usalama ya  mkoa huo Bw, Ezekiel Ruben Magesa mkurugenzi wa mgodi huo  alikubali kuhamisha mali zake zote ndani ya siku 30 ili kupisha eneo hilo licha ya kukataa kusaini makubaliano hao kwa njia ya maandishi.

Nae mkurugenzi wa Mgodi huo Ezekiel Ruben Magesa amesema amekuwa akimiliki eneo hilo  na kulipia mapato  tangu mwaka 1984 kabla ya mgodi wa GGM kuanza shughuli zake katika mkoa huo na kwamba anashangazwa na serikali kuwafukuza katika eneo hilo.

Aidha Radio Kwizera imepiga kambi katika eneo hilo na baada ya masaa 24 kupita, imeshuhudia eneo la mgodi likiwa limezungukwa na maaskari wa jeshi la polisi  ambapo hadi sasa hakuna mtu wakuweza kuingia katika eneo hiloPost a Comment

0 Comments