habari Mpya


Umoja wa chama cha Madereva jijini Mwanza wajiunga na NHIF.

Pichani wapili  kutoka kulia ni Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Jijini Mwanza Mary  Tesha
MWANZA: NA KOSTA KASISI.
Umoja wa Madereva jijini Mwanza umejiunga Mfuko wa Bima ya Afya Taifa NHIF ili kupata matibabu kwa urahisi pale anapo ugua. 
Pichani ni Madereva wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mary  Tesha.
Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mary  Tesha akimwakilisha  Mkuu wa mkoa wa Mwanza  Bw John Mongella ametoa Kadi za Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa  kwa madereva na makondakta katika mkoa wa Mwanza.
 
Akizumgumza katika utoaji huo wa kadi amesem kuwa maendeleo ya Taifa lolote huletwa na watu wenye afya hivyo jambo walilo lifanya madereva hao nimfano wa kuigwa na jamii yote ya watanzania.
Amewapongeza kwa uamuzi wao huo hali ambayo itachangi kufanya kazi zao kwa amani bila ya ya kuhofia gharama za matibabu.

Kaimu meneja NHIF mkoa wa Mwanza amesemakuwa mfuko huo una lengo la kuwafikia wajasiliamali na watanzania wengi kwa wakati kwa mpaka sasa asilimia 70 ya watanzania hawana bima za afya.
Post a Comment

0 Comments