
Bingwa
Mtetezi wa Kombe la Dunia 2014,Ujerumani imekosa kuutetea Ubingwa wake baada ya
kuchapwa magoli 2-0 na Korea Kusini katika mchezo wa Kundi F June 27, 2018 wa Kombe
la Dunia Uwanja wa Kazan Arena nchini Urusi.
Mabao yamefungwa na Kim Young-Gwon dakika ya 90+4 na Son Heung-Min
dakika ya 90+7.


Hii ni mara
ya kwanza ndani ya miaka 80 kwa Ujeruman kutolewa katika hatua ya makundi
ya kombe la Dunia.
Nayo Sweden
imeichapa 3-0 Mexico, mabao ya Ludwig Augustinsson dakika
ya 50, Andreas Granqvist kwa penalti dakika ya 62
na Edson Álvarez aliyejifunga dakika ya 74.
Mexico sasa
inaungana na Sweden kwenda hatua ya 16 Bora na Watacheza kwa Brazil v Mexico na
Sweden v Switzerland.

0 Comments