habari Mpya


Soma Habari June 30,2018-Radio Kwizera FM-Ngara/Kagera.

Hivi karibuni Mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salum Mustapha Kijuu amewaagiza wakuu wa wilaya kuhakikisha wanaweka mikakati ya kudhibiti utoro wa wanafunzi kwa kuwa ni moja ya sababu zinazochangia tatizo na ongezeko la mimba kwa wanafunzi wa kike kufuatia  wanafunzi 231 kupata ujauzito kuazia mwaka 2014 hadi 2018.–Picha Na Maktaba Yetu.Source; RK, WM (mimba za utotoni)
Ed: FM
Date: Friday, June 29, 2018

MISSENYI

Jumla ya wanafunzi 36 wakiwemo 7 wa shule za msingi na 26 katika shule za sekondari wamekatishwa masomo yao baada ya kupata ujauzito kwa kipindi cha mwaka 2015 hadi 2018 wilayani Missenyi Mkoani Kagera

Hayo yameelezwa na afisa elimu sekondari Wilayani humo Bi Saverina Misinde wakati akiwasilisha taarifa ya hali ya matukio ya mimba za utotoni wilayani humo katika kikao cha uzinduzi wa kampeni ya kuzuia mimba za utotoni na mapambano dhidi ya maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi

Amesema vitendo vya kuwasababishia mimba  wanafunzi vimekithiri kwa shule za msingi na sekondari na kusababisha kukatisha ndoto za maisha ya watoto hao  na kwamba ili  vitendo hivyo viweze kukomeshwa  jamii  inapaswa kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola 

Insert ….. Bi Misinde
Cue in ……
Cue out …….

Kwa upande wake mratibu wa kampeni hiyo Respicius John amesema kampeni hiyo imelenga kutokomeza mimba za utotoni kupitia mikutano ya hadhara, mashindano ya michezo, semina juu ya fursa za kiuchumi pamoja na elimu rika ili kuwasaidia vijana kutojiingiza katika mahusiano ya kimapenzi kabla ya umri


Source; RK, KK (Moto)
Ed: FM
Date: Friday, June 29, 2018

MWANZA

Baadhi ya wakazi wa Kata ya Mkolani wilayani Nyamagana   Jijini Mwanza wameiomba Serikali kuboresha Kitengo cha Zima Moto kutokana na kuwepo kwa vitendea kazi vichache pamoja na kuchelewa kufika katika Maeneo ya Matukio

Wamebainisha hayo mara baada ya Moto kutokea June 27 mwaka huu katika kata hiyo na kuteketeza Maghara Mawili ambayo yalikuwa na vitu vya wafanyabiashara yakiwemo Magodoro, Vigae na Mabati

Wamesema mara baada ya moto kuanza walianza juhudi za kuuzima kitendo ambacho hakikuzaa matunda huku gari la zima moto likichelewa kufika katika eneo la tukio ambapo wameiomba serikali kuongeza magari ya zima moto katika maeneo mbali mbali

Insert…………WANANCHI
Ceu in…………
Ceu out………….

Kaimu Kamanda wa Kikosi cha Zimamoto Mkoa wa Mwanza Bw Julius Bulambu amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba uchunguzi wa ajali hiyo unaendelea huku akitoa Rai kwa wananchi kutoa taarifa mapema kwa jeshi hilo pindi tukio linapotokea

Insert…………Kamanda Julius
Ceu in…………..
Ceu out……..

Source; RK, GM (uchunguzi)
Ed: FM
Date: Friday, June 29, 2018
GEITA
Serikali Mkoani Geita imeanza kuwachunguza watendeji wa serikali waliojimilikisha vibanda vya biashara katika soko jipya la Geita baada ya kukiuka utaratibu wa umiliki vibanda hivyo
Akizungumza na wajasiriamali mkoani humo, Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robart Gabriel amesema vibanda hivyo vimejengwa kwa ajili ya wafanyabiashara na wajasiriamali wadogo pekee kutoa fursa ya kutangaza bidhaa zao
Amesema hatua hiyo imekuja baada ya kutembelea katika soko hilo   na kukuta wamiliki wa vibanda wengi wao ni watumishi wa serikali, jambo linalowanyima fursa wajasiriamali wadogo kutangaza bidhaa zao
Insert…………..mkuu wa mkoa.
Cue in………….
Cue out……….
Nae meneja wa SIDO mkoa wa Geita Japhary Donge amewataka wajasiriamali hao kutumia fursa zinazowazunguka katika kujipatia kipato na kuahidi kushirikiana nao kufikia uchumi wa kati kwa kutumia teknolojia rahisi

Source; RK, AK (afya)
Ed: FM
Date: Friday, June 29, 2018

BUKOBA
Jumla ya watoto laki 6 mia 371 wanatarajiwa kupatiwa dawa za minyoo ya Tumbo na kichocho mkoani Kagera kwa mwaka 2017/18
Mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jeneral mstaafu Salum Mustafa Kijuu amesema hayo akizungumza na wajumbe wa kamati ya huduma ya afya msingi mkoani humo
Amesema mpango wa kugawa dawa hizo umeanza na ni jukumu la kila kiongozi kwenye maeneo husika kuwahamasisha wazazi ili watoto wote wanaolengwa na mpango huo waweze kufikiwa
Insert………..Salum Kijuu
Cue in……….
Cue out……..
Kwa upande wake mratibu wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele mkoani Kagera Bw Gervas Ishengoma amesema magonjwa hayo yanaathari kubwa kwani yanaweza kusababisha maudhurio hafifu ya mtoto shuleni, kudhoofisha mwili na muda mwingine kupelekea vifo

Source; RK, EZ (uchomaji moto)
Ed: FM
Date: Friday, June 29, 2018

CHATO

Chama cha mapinduzi CCM Wilayani Chato Mkoani Geita kupitia jumuiya ya wazazi kimesema kitawachukulia hatua za kisheria watendaji wa serikali watakaoshindwa kusimamia vyema utunzaji wa mazingira

Akiongea kwa niaba ya katibu wa jumuiya hiyo wilayani humo Bw Kipande Ally Mjumbe wa mkutano mkuu mkoa wa Geita Bw Frank Musa amesema chama kimeweka mikakati kabambe ya kuhakikisha watendaji wa vijiji, kata pamoja na maafisa kilimo wanawaelimisha wananchi juu ya kutotumia moto kusafisha mazingira

Hata hivyo Bw.Frank amesema kuwa kupitia mikutano ya hadhara nilazima wataalamu hao wajikite kutoa elimu kwa wananchi juu ya uhifadhi wa mazingira kwa kuwaelimisha wananchi madhara ya uchomaji moto katika mazingira

Insert...........Frank Musa
Cue in..........
Cue out.........

Baadhi ya wenyeviti wa vitongoji katika kata ya Chato Mkoani Geita wamepongeza hatua hiyo na kusema kuwa kufanya hivyo wananchi watatambua vyema elimu hiyo na kuachana na tabia ya kusafisha mashamba kwa kutumia moto kama ilivyozoeleka kwa baadhi ya maeneo

Post a Comment

0 Comments