habari Mpya


Sherekeheni kwa kushirki pamoja na wasio kuwa na Kitu -Sheik Nuhu Mussa.

Sheikh Nuhu  akimkabidhi Bi Juliana Nyahingi Kiongzi  wa Kiimani na Mama Walezi katika Kituo cha SOS cha Jijini Mwanza.

Na Kosta Kasisi –RK Mwanza.

 Katika kusherekea  sikukuu ya Eid el Fitri Waislam Katika Msikiti wa Ibazi uliopo Mtaa wa Liberty Jijini Mwanza wametoa zawadi mbalimbali  za vyakula kwa  kituo cha kulelea watoto yatima cha SOS  kilichopo kata ya Mahina Jijini Mwanza.

 Akizungumza June 14,2018 Mara baada ya kukabidhi zawadi   hizo Imam wa Msikiti  wa Ibaz  Sheikh Nuhu Mussa amesema kuwa wao kama sehemu ya Jamii imewapasa Kushirikiana na wale wote wenye uhitaji katika Jamii hususani watoto Yatima.
Amesema kuwa ikiwa ni kilele cha siku ya Mwezi mtukufu wa Ramadhani wameamua kutoa vitu mbalimbali kwa lengo la kuwafariji watoto hao  kwa kushiriki nao pamoja sikukuu ya Eid El Fitri kwa kuwapatia vyakula.

Kwa upande wake Meneja Miradi  SOS Mkoa wa Mwanza Bi Doroth Ndege ameushukuru uongozi wa Msikiti huo wa Ibaz kwa kusema kuwa jukumu la kuwalea watoto yatima ni la kila mtu .
Vitu vilivyotelewa ni Mchele Kilo 100,maharage kilo 100,Nyama kilo 20,mafuta ya kupikia lita 40,Sukari Kilo 50 viazi mviringo Kilo 50 na bidhaa Nyingine ambapo Kituo cha SOS uwalea watoto yatima waliofiwa na wazazi wao ama mbao wanatoka katika familia maskini ambazo hazina uwezo wa kumudu matunzo kwa watoto ambapo kwa sasa kinahudumia watoto 61 walioko katika malezi maalumu ya walezi waliopewa mafunzo.

 

Post a Comment

0 Comments