habari Mpya


Mtoano wa 16 Bora Kombe la Dunia 2018- Ni June 30,2018 Argentina vs Ufaransa - Ureno na Uruguay.

Michuano ya Kombe la Dunia 2018 jana June 28, 2018  imekamilisha hatua ya makundi huku bara  la Afrika  timu zake zote 5 zikiondoshwa katika hatua ya makundi kutokana na kukosa alama za kutosha kuingia hatua ya 16 bora.
 Timu 16 zilizofuzu hatua ya 16 bora ni Uingereza, Ubelgiji, Argentina, Colombia, Japan, Croatia, Hispania, Ureno, Brazil, Switzerland, Mexico, Ufaransa, Uruguay, Urusi, Denmark na Sweden.

Hatua hii ya mtuano ya  16 bora itaanza Jumamosi June 30,2018  kwa kwa michezo miwili Argentina  kuvaana Ufaransa  huku  Ureno  wakicheza dhidi ya Uruguay.
 Jumapili July 01,2018  Michezo miwili Spain kuumana na Wenyeji Russia huku  Croatia wakicheza dhidi ya Denmark.
 
Jumapili July 02,2018  Michezo miwili Brazil kuumana na Mexico huku  Belgium wakicheza dhidi na Japan.
 
Jumapili July 03,2018  Michezo miwili Sweden kuumana na Switzerland huku  Colombia wakicheza dhidi ya England.

Post a Comment

0 Comments