habari Mpya


Maagizo ya Rais Magufuli Kufuatia Ajali ya Basi na Treni Kigoma.

Ajali hii imetokea June 6,2018 na Watu 10 wamekufa na wengine 28 kujeruhiwa kufuatia Basi namba T 885 DLD la Prince Amida lililokuwa likitoka Kigoma kuelekea Tabora baada ya kugonga na treni ya mizigo mkoani Kigoma katika eneo la makutano ya barabara na reli eneo la Gungu katika Manispaa ya Kigoma Ujiji.

Basi hilo la Prince Amida hufanya safari zake kati ya Mikoa ya Kigoma na Tabora.

 Kamanda wa Polisi wa mkoani Kigoma, ASP Martin Otieno amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kwamba chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva kushindwa kuchukua tahadhali kabla ya kuvuka eneo la reli.
  
Katika salamu zake za maombolezo Rais wa Tanzania Dkt.John Magufuli amesema kwa mara nyingine nchi imepoteza nguvu kazi ya Taifa huku akiwataka wadau wote wa usalama barabarani kuchukua hatua madhubuti kuzuia ajali ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua kali wanaokiuka sheria za usalama barabarani.

Post a Comment

0 Comments