habari Mpya


Kasharara fc na Burigi fc zatoshana nguvu kwa sare 0-0 katika ufunguzi wa ligi ya Omuhoranzi Cup

Muleba na Shafiru Yusufu
Ligi ya Omuhoranzi Cup imeanza kutimua vumbi leo katika kiwanja cha Madalena  kata ya Karambi Wilyani Muleba Mkoani Kagera huku timu za ufunguzi wa ligi hiyo Kasharara fc na Burigi fc zikitoka sare ya bila kufungana.

Ligi hiyo inashirikisha Timu za mpira wa miguu 6 kutoka wilayani Muleba mkoani Kagera.
Akifungua mashindano hayo ambayo yalikuwa yamesubiliwa kwa hamu  Mgeni rasmi Diwan wa kata ya Mazinga Bw.Alex Thadeo amewataka wachezaji pamoja na mashabiki kucheza kwa lengo la kujenga umoja na mshikamano ilikusaidia kujenga kata hiyo.

Naye  mdhaminiwa ligi hiyo ambaye Diwani wa kata hiyo ya Karambi Bw.Felix France  amesema lengo la ligi hiyo ni kuandaa ligi ya Kata ambayo itashidana ngazi ya wilaya.
Kwa upande wao makocha wa Timu zote mbili  wamewakata mashabiki na wadau wa mpira wa miguu kutoa ushirikiano mpaka kuisha kwa ligi hiyo.

Hata hivyo zawadi zitakazotolewa mshidi wa Kwanza atajinyakulia kitita  shilingi laki mbili na elfu ishirini, mshidi wa pili laki moja na elfu hamsini, mshindi wa tatu laki moja na timu yenye nidhamu itapewa zawadi ya shilingi elfu ishirini.

Post a Comment

0 Comments