habari Mpya


Halmashauri ya Muleba wawezesha Ufanisi Mradi wa Vijana KHASAM kijiji cha Buyaga.

Mradi wa Vijana KHASAM kijiji cha Buyaga wilayani Muleba Mkoani Kagera  wakilima  ekari 30 za Passion katika scheme ya Umwagiliaji ya Buyaga na wanatumia miundombinu iliyowekwa na Halmashauri ya wilaya hiyo.
  Pia wana ekari 7 za zao la Nanasi.
Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Kagera ikiongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi, Bi. Constancia Buhiye imetembelea na kukagua miradi ya Maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Muleba ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Mwaka 2015.

Katika ziara hiyo, Kamati ya Siasa ya Wilaya itatembelea na kukagua Ujenzi wa Mradi wa Daraja la Kishara, Mradi wa Umwagiliaji Buhangaza na Buyaga.
Gharama za Mradi waliowekeza ni Shilingi milioni 40 ambapo Halmashauri ya wilaya ya Muleba iliwakopesha kiasi cha Shilingi milioni  21.

Mradi una Jumla ya Vijana 17 ambao wote ni wa Kiume. 

Soko lao  wanauzia Wananchi na wanasafirisha Mtukula wilayani Misenyi ambalo ndilo Soko lao kuu. Mipango ya baadaye ni kuwa na kiwanda cha kukamua Juisi.

Post a Comment

0 Comments