habari Mpya


Gavana wa benki kuu ya Tanzania Profesa Florens Luoga mgeni rasmi katika michuano ya Golf

Na Luteni Selemani Semunyu, JWTZ
Gavana wa benki kuu ya Tanzania Profesa  Florens Luoga anatarajiwa kuwa mgeni Rasmi katika mashindano ya wazi ya golf Tanapa Lugalo open yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Juni 22 katika Viwanja vya Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania wa Lugalo Jijijini Dar es  Salaam.

Hayo yabainishwa na Mwenyekti wa Klabu ya Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania la Lugalo Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo  kupita taarifa nakwamba Gavana huyo Profesa  Florens Luoga amethibitisha kushiriki kufunga mashindano hayo.

Amesema kukubali kwa Gavana Profesa Luoga  kuwa mgeni rasmi katika mashindano hayo ni faraja kwa Klabu ya Gofu ya lugalo ambayo ndio imepewa dhamana ya kuandaa mashindano hayo ambayo yanasomeka katika kalenda ya TGU.
Kwa upande wake mtunza Viwanja Greeen keeper David Helela alisema kazi ya kuweka Alama katika viwanja (Mark() imekamilika na kichachosubliwa sasa ni upangaji wa droo na kutangazwa ili kila mmoja aweze kutambua kuwa yuko katika Nafasi gani na muda gani wa Mchezo

 “Uwanja uko katika hali Nzuri na Wachezaji wanaendelea na mazoezi ya mwisho ili kuhakikisha mashindano yanakuwa mazuri kwa Upande wao na kuibuka na Ushindi mnono”.

Baadhi ya wachezaji wa Vilabu mbalimbali wameonekana katika Viwanja vya Lugalo wakifanya mazoezi ya mwisho kujiandaa na michuano hiyo ambayo kwa ijumaa itaanza kwa Wachezaji wa kulipwa na Wachezaji wasaidizi huku Jumamosi na jumapili ikisalia kwa wachezaji wa ridhaa. 

 Mashindano hayo yatashirikisha  wachezaji wa Ridhaa na wa Kulipwa katika makundi yote ikiwemo Wanawake Wazee na Watoto sambamba na Wachezaji wasaidiizi ambao watapata nafasi katika Siku ya kwanza ya Mashindano.

Mashindano hayo yanayodhaminiwa na  Mamlaka ya Hifadhi za taifa TANAPA ili kuunga mkono Jitihada za Serikali kukuza michezo na gofu ina muunganiko na Utalii hivyo wanaimani kupitia Gofu pia itakuza uchumi kutokana na kukua kwa Utalii.

Mashindano ya  Lugalo open  hufanyika kila mwaka  kwa mujibu wa kalenda ya TGU na Klabu ya JWTZ ya Lugalo imekuwa ikipewa dhamana ya Kuyaaandaa.

Post a Comment

0 Comments