habari Mpya


DED NGARA: WATAALAM WA ARDHI PIMENI MAENEO YA WANANCHI NA NAKUWAPATIA HATI MILIKI.


NAMWANDISHI WETU AMOS JOHN
Pichani watatu kutoka kushoto ni mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ngara mkoani Kagera akiwa katika picha ya pamoja wakati wakufunga mafunzo kwa wakulima yaliyo kuwa yakitolewa na MKURABITA kijiji cha mnjebwe wilayani humo.

Jumla ya wakulima 104 wa kijiji cha munjebwe kata ya Rulenge wilayani  Ngara mkoani Kagera  wamepatiwa elimu  na Shirika la Mkurabita kwa mda wa siku 3 elimu itakayo wa saidia wao kujikwamua kiuchumi na kuondokana na umasikini.


Wakulima hawa ni wale walio rasimisha mashambayo kisheria kutoka katika vijiji viwili wilayani Ngara mkoani Kagera ambavyo ni Buhohoro na Munjebwe.
akizungumza na mwandishi wetu wakati wa hafla ya kuhitimisha mafunzo hayo Mkurugenzi mtendaji wa halimashauri ya Wilaya ya Ngara Bw. Aidani Bahama amewataka wataalamu wanao husika  na ardhi  wilayani humo kuhakikisha wanapima viwanja na kuwapa  hatimiliki wananchi kuanzia ngazi ya vijiji ,kata mpaka tarafa ili wananchi waweze kupata mikopo kwa urahisi

Pichani ni washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia kwamakini wailichokuwa wakiendelea kuelekezwa.
Bw. Bahama ameongeza kuwa  kwasasa Tanzania inaelekea  kwenye uchumi wa viwanda hivyo amewaomba wakulima kulima zao la kahawa kwa wingi maana wakulima ndio nguzo muhimu katika kuelekea  serikali ya viwanda.


Pichani Meneja kutoka ofisi ya Raisi urasimishaji mali Ardhi Tanzania bara Antho Temu akizungumza katika zoezi la kufunga mafunzo hayo.
Meneja kutoka ofisi ya Raisi urasimishaji mali Ardhi Tanzania bara Antho Temu amesema lengo la kutoa elimu kwa wakulima nikuwajengea uwezo kulima kilimo cha kisasa na kuachana na kilimo cha mazoea ikiwa ni pamoja na kuwa hamasisha wakilima kuunda vikundi malimbali ili viwasaidie kujikwamua kiuchumi.
Bw.Temu amesema wamewaelekeza wakulima namna ya utunzaji wa kumbukumbu katika kilimo ilikuwasaidia kutopata hasara katika kilimo chao.

Kwa upande wao baadhi ya wakulima walio patiwa mafunzo hayo wame ushukuru uongozi wa mkurabita kwakuwapa mafunzo yatakayo wawezesha wao kujikwamua kiuchumi huku wakisema kuwa elimu walio ipata  watakwenda kuwaelimisha nawengine ambo hawakupata elimu hiyo na wameshauri mafunzo hayo yawe yanatolewa marakwamara.

Post a Comment

0 Comments