habari Mpya


CCM WILAYANI KAHAMA YAKANA TAARIFA ZA LEMBELI KURUDI NDANI YA CHAMA HICHO.

Pichani ni Katibu wa itikadi na uenezi wa chama cha mapinduzi CCM wilayani Kahama mkoani Shinyanga Bw.Joakimu Simbira akizungumza na wanahabari.
Na mwandishi wetu Simoni Dionizi
Chama cha mapinduzi CCM wilayani Kahama mkoani shinyanga kimekana kuwa hakimtambui James Lembeli aliye wahi kuwa mbunge wa jimbo la Kahama toka mwaka 2005 hadi 2015 kupitia CCM kama mwanachama wa chama hicho na hakijapokea taarifa za yeye kuhamia nadani ya chama hicho.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa itikadi na uenezi wa CCM  wilayani Kahama mkoani Shinyanga Bw.Joakimu Simbira wakati akizungumza na waanshi wa habari ambapo ameongeza kuwa James Lembeli amekurupuka hajafuta taratibu hivyo chama hakiwezi kufanyia kazi taaria ambazo zinakiuka utaratibu wa chama. 

Chama cha Mapinduzi kinataratibu zake hivyo sisi kama chama hatuna taarifa sahihi za Lembeli kujiunga na chama chetu amekurupuka tu hivyo hatumtambui”Amesema Simbira.
Hata hivyo Bw.James Lembeli alipo tafutwa na wanahabari kwanjia ya Sim hakuwa tari kupokea simu ambapo hadi habari hii inakufikia wewe msomaji Lembeli hakuwa tayari kupokea Simu.
James Lembeli aliye wahiku Mbunge wajimbo la Kahama kabla ya kuhamia chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema mwaka 2015 nakushindwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka huo kwasasa alitangaza kurudi CCM.
  


Post a Comment

0 Comments