habari Mpya


Watu 12 wamefariki Dunia Ajali ya Basi la City Boys kugongana uso na fuso Tabora.

Muonekano wa Basi la City Boy baada ya Ajali.

Watu 12 wamefariki dunia baada ya basi la abiria la City Boys lililokuwa likitokea wilayani Karagwe mkoani Kagera kwenda Dar es Salaam, kugongana uso na fuso katika eneo la kijiji cha Makomero wilayani Igunga Mkoa wa Tabora usiku wa kuamkia leo April 5, 2018.

Mkuu wa Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, John Mwaipopo, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa ajali hiyo imesababisha majeruhi 46 ambao wanapatiwa matibabu katika hospitali ya wilaya hiyo.
Mabaki ya Basi la City Boy lililokuwa linatoka Wilayani Karagwe mkoani Kagera kwenda Jijini Dar es Salaam na kugongana uso kwa uso.
Lori aina ya Fuso lililopoteza mwelekeo na kulifata Basi hilo la City Boy lililokuwa linatoka Wilayani Karagwe mkoani Kagera kwenda Jijini Dar es Salaam na kugongana uso kwa uso.

Post a Comment

0 Comments