habari Mpya


Safari ya Mtoto Anthony Petro wa Ngara mkoani Kagera kwenda Masomoni mkoani Kilimanjaro.

Na Shaaban Ndyamukama-Radio Kwizera Ngara.

Safari ya Mtoto Anthony Petro wa Ngara mkoani Kagera ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Bw.Aidan Bahama ya kwenda masomoni katika shule ya Amani Humwe wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro imeanza leo April 8,2017 baada ya kumpata mfadhili wa kumsomesha.

Akionesha nyuso ya furaha kwenye safari yake mtoto Anthony amesema anakwenda shule kutimiza ndoto ya kusaidia familia akitaka apate kazi yenye maana.

Ameahidi kufanya vizuri atakapokuwa darasani akisisitiza baba yake na dada zake wawili wahamishwe kuweza kuishi sehemu yenye usalama " Mimi sijui hata kiingereza nikienda hiyo shule watanifundisha niwe naongea kama wazungu"
Safari ya Mtoto Anthony Mtoto anapelekwa shuleni na Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Ngara, Aidan Bahama, aliyeambatana pia na Afisa Ustawi wa Jamii Bw.Musa Balagondoza.

Mtoto Anthony anatarajiwa kukabidhiwa kwa mfadhili wake Isihaka Msuya ambaye ameahidi kugharimikia kila kinachohitajika kitaaluma.

Aidha  halmashauri ya wilaya ya Ngara  itakuwa mfuatiliaji kila hatua ikiwa ni pamoja na kumfuata au kumpeleka kwa usafiri salama wakati na baada ya likizo za kila muhula. 

Bi. Stella Rutaguza ambaye anaratibu michango ya kumsaidia Mtoto Anthony mkoani Dodoma kutoka kwa Watanzania wanaoguswa wa ndani na nje ya Ngara,Hadi sasa amepata sh2.2 million huku fedha taslimu zikiwa ni Sh1.37 milioni

Post a Comment

0 Comments