habari Mpya


Mwenge wa Uhuru wapokelewa Kagera ,kuzindua Miradi 65 yenye Thamani ya Shilingi Bilioni 12.38.

Picha na Shafiru Yusuf- Radio Kwizera Muleba.

Mwenge wa Uhuru umepokelewa leo April 8, 2018 Mkoani Kagera na Mkuu wa Mkoa Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabrie Luhumbi katika Kijiji cha Nyakabango  mpakani mwa mkoa wa Kagera na Geita.

 Mkoa wa Kagera Mwenge wa Uhuru unatarajia kupitia Jumla ya miradi 65 yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 12.38.

Katika miradi hiyo 65 Mwenge wa Uhuru Utazindua miradi 33, utakagua miradi 15, Utaweka mawe ya msingi katika miradi 13 pamoja na miradi 19 ambayo itatembelewa na kukaguliwa.
Aidha, mchanganuo wa gharama za miradi hiyo 65 itakayopitiwa na Mwenge wa Uhuru 2018 Serikali kuu imechangia kiasi cha shilingi 5.81 sawa asilimia 47%.

Halmashauri za wilaya zimechangia zaidi ya shilingi milioni 671 sawa na asilimia 6 ,Wahisani wamechangia shilingi Bilioni 3.7 sawa na asilimia 30 na Wananchi wa Mkoa wa Kagera wamechangia shilingi Bilioni 2.1.
Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2018 zinaongozwa na Bw. Charles Kabeho kutoka mkoa wa Dar es Salaam akishirikiana na Bw. Issa Abasi Mohamed (Kusini Pemba), Bi. Agusta Safari (Geita), Bw. Ipyana Mlilo (Tanga), Bw. Dominick Njunwa (Kigoma) na Bi. Riziki Hassan Ali (Kusini Unguja).

Mwenge wa Uhuru utakimbizwa umbali wa takribani kilomita 103,440.7 kwa siku 195 katika mikoa yote 31 nchini na halmashauri za wilaya 195 na Kaulimbiu ya mbiu za Mwenge kwa mwaka huu ni Elimu ni ufunguo wa maisha, wekeza sasa kwa maendeleo ya Taifa letu.’

Post a Comment

0 Comments